Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hivi Karibuni Utaweza Kuunganisha WhatsApp na Instagram

WhatsApp kuja na Njia mpya ya kuunganishwa na Instagram
Whatsapp kuunganishwa na Instagram Whatsapp kuunganishwa na Instagram

Tokea mwaka 2012 Facebook iliponunua mtandao wa Instagram kwa dollar za marekani bilioni $1 sawa na zaidi ya Tsh Trilioni 2.2. Facebook imekua na jitihada kubwa kuhakikisha mtandao huo unaunganishwa na programu nyingine kutoka kampuni ya Facebook.

Kuonyesha hilo, hivi leo habari kutoka kwenye mitandao mbalimbali ya Habari za teknolojia zinasema kuwa,  Facebook ambayo ndio kampuni miliki ya programu za WhatsApp na Instagram imepanga kuleta sehemu mpya ambayo itakuwa inakuwezesha kuunganisha akaunti yako ya Instagram pamoja na namba yako ya WhatsApp.

Advertisement

Kupitia mtandao wa Wabetainfo ambao unatoa habari mbalimbali kuhusu ujio wa sehemu mpya kwenye programu ya WhatsApp, hivi leo umeandika kuwa sehemu hiyo inaonekana kuwepo kwenye hatua za majaribio na siku sio nyingi huenda sehemu hiyo ikaja rasmi kwanza kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp ya biashara.

https://twitter.com/theinformertz/status/1052968608748490752

Kupitia sehemu hiyo mpya watumiaji wa programu ya WhatsApp ya biashara watakuwa na urahisi wa kuweza kuwa onyesha wafuatiliaji wao akaunti zao za Instagram pia njia hii italeta urahisi kwa Instagram kuweza kufanya Verification ya kurasa mbalimbali za mtandao wa Instagram.

Kwa sasa kama nilivyosema sehemu hii iko kwenye hatu za majaribio hivyo siku sio nyingi tutasikia mengine mengi kuhusu sehemu hiyo mpya.

Mbali na hayo WhatsApp pia inafanyia kazi sehemu mpya ya Silent Mode, sehemu ambayo hii itakuruhusu kuzima zile namba zinazotokea mbele ya chat za group au mtu mmoja mara baada ya kutumiwa meseji, namba hizo hutokea ikiwa inaonyesha idadi ya meseji mtu au group ulizopokea. Sehemu hiyo ya Silent Mode itaweza ku-mute meseji pamoja na namba hizo na zitaweza kuzima hadi zile namba zenye kuonyesha idadi ya meseji zilizongia kwenye chat fulani. Sehemu hiyo nayo iko kwenye hatua za majaribio hivyo pengine inaweza kutoka rasmi pamoja na sehemu hiyo mpya ya kuunganisha akaunti hivyo kwa habari zaidi za sehemu hizi endelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use