Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tecno Yazindua Tecno Camon iClick 2 Maalum Kwa Nchini India

Simu mpya ya Tecno yenye ukingo wa juu pamoja na mfumo wa AI
Sifa na Bei ya Tecno Camon iClick 2 Sifa na Bei ya Tecno Camon iClick 2

Kampuni ya Tecno inajulikana sana kwa uuzaji wa simu za bei nafuu kupitia nchi mbalimbali, moja ya soko ambalo pia kampuni ya Tecno inaonekana kupendwa zaidi ni pamoja na soko la nchini India ambapo kampuni ya Tecno hivi karibuni imezindua simu mpya ya Tecno Camon iClick 2.

Simu hii ambayo pengine itakuja nchini Tanzania ikiwa na Jina lingine, inakuja na mfumo wa AI kwenye kamera zake hivyo ni sawa kusema simu hii inakuja na uwezo mzuri sana wa kamera kama zilivyo simu nyingi za Tecno Camon.

Advertisement

Simu hii ya Tecno Camon iClick 2 inakuja na kioo cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa HD Full View ambacho pia kinakuja na ukingo wa juu maarufu kama notch, Simu hii pia inakuja na processor ya MediaTek Helio P22 yenye uwezo wa octa-core processor yenye speed ya 2GHz ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64, Tecno iClick 2 inaweza kuongezewa ukubwa wa ndani kwa kutumia memory card hadi yenye uwezo wa GB 128.

Simu hii ambayo ni maalum kwa nchini india inakuja na kamera ya mbele yenye uwezo wa Megapixel 24, huku ikiwa na teknolojia ya AI ambayo inafanya mtumiaji aweze kupiga picha zenye mvuto zaidi, huku kwa nyuma simu hii ikiwa inakuja na kamera mbili ambayo kamera moja inakuja na uwezo wa Megapixel 13 na nyingine ikiwa na uwezo wa Megapixel 5 huku zote kwa pamoja zikiwa na sehemu mpya za Super Pixel na AI Bokeh ambazo hufanya picha hasa za portrait mode kuwa angavu zaidi. Sifa nyingine za Tecno Camon iClick 2 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Camon iClick 2

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya HD IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1500 X 720 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) yenye mfumo wa HiOS 4.1
  • Uwezo wa Processor – 2.0GHz Octa-Core.
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek Helio P22 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 509.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye 1.8um pixel, f/2.0 aperture, na flash
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.8 na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.4. Huku zote zikiwa zinasadiwa na bokeh Mode, AI HDR, AI Beauty, Panorama pamoja na LED tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3750 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa m za Gloss midnight blue
  • Mengineyo – Bado haijajulikana kama inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass na AI Face Unlock.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma) na Face Unlock.

Bei ya Tecno Camon iClick 2

Kwa upande wa bei kama nilivyo sema awali simu hii ni maalum kwa nchini India hivyo itakuwa inapatikana nchini India kwa Rupee Rs 13,499 sawa na Tsh 417,000 bila kodi. Simu hii inaweza kuja nchini Tanzania lakini tegemea kuipata ikiwa kwa jina lingine. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kwa nchini Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use