in

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Nokia 3.1 Plus

Toleo jipya la simu ya Nokia 3.1

Hizi hapa sifa na bei ya Nokia 3.1 Plus

Kampuni ya Nokia hivi leo imetangaza toleo jipya la simu mpya ya Nokia 3.1 Plus, Simu hii inakuja na maboresho ya kamera, sehemu ya fingerprint na pia inakuja na kioo kikubwa kuliko toleo la Nokia 3.1 toleo ambalo limetoka miezi kadhaa iliyopita.

Nokia 3.1 Plus inakuja na kioo cha inch 6.0 chenye resolution ya 720 x 1440 pixel na kioo hicho hakina ukingo wa juu maarufu kama notch. Simu hii inakuja na kamera ya mbele yenye Megapixel 8 pamoja na kamera za nyuma zenye Megapixel 13 pamoja na Megapixel 5.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Nokia 3.1 Plus inaendeshwa na processor ya MediaTek Helio P22 yenye uwezo wa Octa-core Cortex-A53 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 2 au GB 3. Simu hii pia inakuja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 16 au GB 32 huku ukiweza kuongezea ukubwa huo wa kutumia Memory Card hadi ya GB 400. Nokia 3.1 Plus inatumia mfumo wa Android One (Oreo) mfumo ambao utaweza ku-update siku za karibuni kwenda kwenye mfumo mpya wa Android 9 (Pie). Sifa nyingine za Nokia 3.1 Plus ni kama zifuatazo.

Sifa za Nokia 3.1 Plus

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1440 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~268 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) inaweza ku-update hadi Android 9 Pie (Android One)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6762 Helio P22 (12 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 16 na nyingine inakuja na GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 3 na nyingine ikiwa na GB 2.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.2.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/2.0, AF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.4, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na HDR na LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.1 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Blue, White na Gray.
  • Mengineyo – inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Nokia 3.1 Plus

Simu hii mpya ya Nokia 3.1 Plus inategewa kupatikana kuanzia siku ya leo huko nchini india kuanzia rupee ya India INR 11,500 sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 357,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kupanda au kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Nokia 3.1 Plus
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.