Kampuni ya Dell Yazindua Laptop Mpya ya Dell Inspiron 7572

Zifahamu hapa sifa na bei ya laptop mpya ya Dell Inspiron 7572
Dell inspiron 7572 Dell inspiron 7572

Kampuni ya Dell hivi karibuni imerudi tena na laptop yake mpya ya Dell Inspiron 7572, laptop hii inakuja na kioo cha inch 15.6 kilichotengenezwa kwa teknolojia ya FHD chenye resolution ya 1920 x 1080 ambacho pia ni InfinityEdge IPS display.

Kava la laptop hii limetengenezwa kwa ubora kwa kutumia Aluminum pamoja na Magnesium alloy, ambayo kwa pamoja inafanya laptop hii kuwa na kava lenye ubora zaidi. Kwa ndani Dell Inspiron 7572 inakuja na processor ya Intel Core i5-8250U processor yenye speed ya 3.4GHz ambayo inasaidiwa na RAM ya DDR4 yenye uwezo wa GB 8. Vilevile laptop hii inakuja na toleo lingine lenye processor ya Intel Core i7-8550U processor yenye speed ya 4.0GHz.

Kwa upande wa Graphics, laptop hii inakuja na GPU ya NVIDIA GeForce MX150 yenye uwezo wa GB 4 GDDR5 graphics memory. Mbali na hayo Dell Inspiron 7572 inakuja na ukubwa wa kuchagua kati ya SSD yenye ukubwa wa GB 128 au HDD yenye ukubwa wa TB 1, sifa kamili za Dell Inspiron 15 7572 ni kama zifuatazo.

Advertisement

JinaDell Inspiron 7572
Ukubwa19.5 x 358.16 x 246.95mm
Uzito2.00kg
Kioo15.6-inch FHD (1920 x 1080)
CPU8th Generation Intel Core i5-8250U/ i7-8550U
GPUNVIDIA GeForce MX150
RAM8GB – expandable upto 16GB
Ukubwa wa ndani128GB SSD + 1TB
Sehemu za kuchomeka1 HDMI, 1 USB 3.0, 1 USB 3.0 with PowerShare , 1 USB 2.0, 1 Noble lock slot, 1 SD card
Battery42 WHr
Mfumo wa uendeshajiWindows 10 Home/Pro

Bei ya Dell Inspiron 7572

Kwa upande wa bei ya Dell Inspiron 7572 inatarajiwa kuuzwa kwa nchini india na itakuwa inapatikiana rasmi kwa matoleo manne tofauti ambapo toleo la chini litapatina kwa rupee ya india RS 54990 ambayo ni sawa na Tsh 1,715,000 bila kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use