Sifa na Bei ya Huawei Mate 20 na Huawei Mate 20 Pro

Fahamu kwa undani hizi hapa ndio sifa na bei ya simu mpya za Huawei Mate 20
Sifa na Bei ya Huawei Mate 20 na Mate 20 Pro 1 Sifa na Bei ya Huawei Mate 20 na Mate 20 Pro 1

Kampuni ya Huawei tayari imesha zindua simu zake mpya za Huawei Mate 20 na Huawei Mate 20 Pro, kama ilivyokuwa kwenye tetesi simu hizi za Huawei zimefanyiwa maboresho mengi sana ukitofautisha na simu za mwaka jana za Huawei Mate 10.

Kwanza simu hizi mpya za Huawei Mate 20 na Huawei Mate 20 Pro zinakuja zikiwa zinaendeshwa na processor mpya kutoka Huawei za Kirin 980 ambazo pia zimeongezewa mfumo wa AI na AR hivyo kufanya simu hizo kuwa za kisasa zaidi. Mbali na hayo Huawei imekuja na teknolojia mpya ya kuchaji simu hizo kwa haraka kwa kuja na njia mpya ya kuchaji simu hiyo hadi asilimia 70 kwa muda wa nusu saa tu, mbali na hayo yafuatayo ndio mambo mengine unayotakiwa kujua kuhusu Simu hizi mpya za Huawei Mate 20 na Mate 20 Pro.

Huawei Mate 20

Advertisement

Huawei Mate 20 inakuja na kioo cha inch 6.53 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya LCD chenye resolution ya 1080 x 2244 pixels. Kwa mbele Mate 20 inakuja na kamera ya Megapixel 24 ambayo iko kwenye ukingo wa juu maarufu kama notch. Simu hii inaendeshwa na processor ya Krin 980 ambayo kama nilivyo sema inakuja na teknolojia ya AI pamoja na AR au Augmented Reality.

Kwa nyuma Mate 20 inakuja na kamera tatu, kamera ya kwanza inakuja na Megapixel 12 ambayo hii ndio kamera ya kawaida nyingine inakuja na uwezo wa Megapixel 16 ambayo hii ni wide angle na kamera ya mwisho inakuja na uwezo wa Megapixel 8 ambayo hii ni Telephoto, kamera zote zinakuja na mfumo wa AI.

Mbali na hayo Huawei Mate 20 inakuja na battery kubwa ya 4,000mAh yenye teknolojia ya Fast charge pamoja na simu hii inakuja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, sifa nyingine za Huawei Mate 20 ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei Mate 20

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.53 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2244 pixels, na uwiano wa 18.7:9 ratio (~381 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa Huawei EMUI 9.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.6 GHz
  • Aina ya Processor (Chipset) – Huawei Kirin 980 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP10.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja inakuja na RAM ya GB 6 na nyingine inakuja na RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 27mm, 1/2.3″ na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/2.2, 17mm (wide lens), na nyingine inakuja na Megapixel 8 yenye f/2.4, 52mm (telephoto lens). Huku zote zikiwa zinasadiwa na Leica optics, panorama, HDR pamoja na flash ya dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging yenye uwezo wa kuchaji asilimia 58 kwa nusu saa.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tano za Emerald Green, Midnight Blue, Twilight, Pink Gold na Black.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, barometer, na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Huawei Mate 20 Pro

Kwa upande wa Huawei Mate 20 Pro yenyewe ni tofauti kidogo na Mate 20 kwani inakuja na kioo cha inch 6.39 ambacho ni Curved display kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED OLED chenye resolution ya 1440 x 3120 pixels. Kwa mbele Mate 20 Pro inakuja na kamera ya Megapixel 24 ambayo kwa pembeni yake kuna sensor ya kutambua uso maarufu kama 3D face scanner.

Kwa nyuma Huawei Mate 20 Pro inakuja na kamera tatu za Megapixel 40 ambayo ni wide angle lens, nyingine inakuja ni Megapixel 20 ambayo hii ni ultra wide na nyingine ni Megapixel 8 ambayo hii ni telephoto lens zote zikiwa na teknolojia ya AR pamoja na AI.

Mbali na kamera Huawei Mate 20 Pro inakuja na battery kubwa ya 4200mAh yenye teknolojia ya fast charging. Simu hii pia inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi ikiwa na uwezo wa kukaa kwa muda wa nusu saa kwenye maji ya mita mbili. Mate 20 Pro nayo inatumia processor ya Kirin 980 yenye teknolojia za AI pamoja AR. Sifa nyingine za Huawei Mate 20 Pro ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei Mate 20 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.39 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 3120 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~538 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa Huawei EMUI 9.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.6 GHz
  • Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 980 (7 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP10.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye f/2.0, 26mm (wide)
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 40 yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/1.7″, PDAF/Laser AF na nyingine ikiwa na Megapixel 20 yenye f/2.2, 17mm (ultra-wide), 1/2.7″, PDAF/Laser AF, na nyingine inakuja na Megapixel 8 yenye f/2.4, 80mm (telephoto), 1/4″, 5x optical zoom, OIS, PDAF/Laser AF. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Leica optics, panorama, HDR pamoja na flash ya dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4200mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging yenye uwezo wa kuchaji asilimia 70 kwa nusu saa.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tano za Emerald Green, Midnight Blue, Twilight, Pink Gold na Black.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbu (IP68) inauwezo wa kukaa kwa muda wa nusu saa kwenye maji ya mita 2.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, barometer na compass
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwenye Kioo kwa Mbele).

Bei ya Huawei Mate 20 na Huawei Mate 20 Pro

Kwa upande wa bei Huawei Mate 20 yenyewe imetangazwa kuja kwa matoleo mawili, toleo lenye RAM ya GB 4 na ukubwa wa ndani wa GB 128 litauzwa kwa Euro €800 sawa na Tsh 2,123,000 bila kodi. Toleo lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 128 litauzwa kwa Euro €850 sawa na Tsh 2,256,000 bila kodi. Kwa upande wa Huawei Mate 20 Pro yenyewe inakuja kwa toleo moja lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 128 ambalo litauzwa kwa Euro €1,050 sawa na Tsh 2,787,000 bila kodi.

Simu hizi za Huawei Mate 20 na Mate 20 Pro zinategemewa kuanza kupatikana kuanzia siku ya leo, huku matoleo mengine ya Huawei Mate 20 X na Mate 20 Porsche yakitegemewa kupatikana kuanzia mwezi october 26 mwaka huu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use