in

Mabadiliko Mapya Yanayokuja Kwenye Programu ya WhatsApp

Hivi karibuni utaweza kuona matangazo kwenye App ya WhatsApp

matangazo kwenye WhatsApp

WhatsApp imekuwa ikifanyiwa maboresho karibia kila mwezi, lakini hivi karibuni mabadiliko mapya yanayokuja kwenye programu ya WhatsApp ni ya tofauti kidogo na mabadiliko mengine. Mabadiliko hayo mapya yanahusiana na chanzo cha mgunduzi wa WhatsApp kuamua kuachana na kampuni ya Facebook ambayo kwa sasa ndio inayomiliki programu hiyo maarufu ya kuchat duniani.

Kama wewe ni mmoja wa wafuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tech lazima utakuwa umesoma makala juu ya mmoja wa wagunduzi wa WhatsApp kuachana na kampuni ya Facebook na baadae kutangaza kwa wafuasi wake kwenye mtandao wa Twitter huku akiwahitaji wafute mtandao huo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao walikuwa hawajui sababu ya mgunduzi huyu kusema maneno hayo na kuachana na kampuni ya Facebook basi nitakwambia leo. Miaka kadhaa iliyopita waanzilishi hao waligundua programu ya WhatsApp kipindi hicho kama unakumbuka vizuri njia iliyokuwa inatumika na wagunduzi hao kujipatia pesa ni pamoja na watumiaji kulipia dollar $0.99 sawa na Tsh 2,289 kwa mwaka kwa ajili ya kutumia programu ya WhatsApp.

Mara baada ya Facebook kununua App hiyo sehemu hiyo ilitolewa kabisa na WhatsApp ilibaki kuwa programu ya bure kwa asilimia 100. Lakini sasa hivi karibuni kumetokea kutoelewana kwa Facebook na mwazilishi huyo mweza wa programu ya WhatsApp mara baada ya Facebook kutaka kuanza kuonyesha matangazo kupitia App ya WhatsApp. Kama alivyo hojiwa na tovuti ya Forbes mwazilishi huyo alisema kuwa, mpango wa Facebook kutaka kuonyesha matangazo kwenye App hiyo kunatofautiana na sababu ya wao kuanzisha app hiyo hivyo haoni haya ya kuendelea kufanya kazi chini ya kampuni hiyo inayo kinzana na sababu zake.

Mpango wa Facebook ni kuja na njia mpya ambayo sasa watumiaji wa App ya WhatsApp watakuwa wanaona matangazo kwenye programu hiyo, najua unajiuliza ni sehemu gani matangazo hayo yatakuwa yanaonekana.? Sasa kwa mujibu wa tovuti ya express.co.uk ambayo lithibitsha hayo kwa kufanya mahojiano na mmoja wa wafanyakazi wa Facebook aliandika kuwa, Hadi kufikia mwaka 2019 WhatsApp itakuwa ikionyesha matangazo kupitia sehemu ya Status ambayo inaonyesha video kwa sekunde kadhaa.

Bila shaka kubadilika huku kwa whatsApp kutakuwa ni pigo kubwa sana kwa watumiaji wa WhatsApp, lakini pengine kwa watu wengine hasa wafanyabiashara hii itakuwa ni habari njema kwani sasa wataweza kuwafikia wateja wengi zaidi kupitia programu hiyo.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za lini sehemu hiyo itakuja rasmi kwenye programu ya WhatsApp ila mpaka 2019 tegemea kuanza kuona matangazo kwenye programu ya WhatsApp kama ilivyo programu za Facebook na Instagram. Hebu tuambie wewe onaonaje hii imekaa poa au..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Mabadiliko Mapya Yanayokuja Kwenye Programu ya WhatsApp
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2024)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments

  1. Kwa upande wa izo ads wanazotaka kuongeza ikiwa seemu ya matangazo kweny status itakuwa ni bored kwa sis ambao sio wafany biashara japo kwa upande mwingine watafaidika wenye biashar kama mlivyosema.. na wasap c itakuwa ya kulipia tena au for free??