Baada ya kampuni ya Samsung kuja na simu mpya ya Galaxy A7 (2018) yenye kamera tatu kwa nyuma, hatimaye hivi karibuni Samsung imeamua kuongeza ubunifu zaidi kwa kuja na Galaxy A9 (2018) simu ya kwanza kutoka kampuni ya Samsung yenye kamera nne kwa nyuma.
Japo kuwa upatikanaji wa simu hii bado ni tetesi lakini kwa mujibu wa tovuti mbalimbali za teknolojia kuna uwezekano mkubwa sana kwa simu hii kuingia sokoni hivi karibuni. Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena hivi karibuni kumevuja nyaraka muhimu ambayo inaonyesha simu hiyo kwa nyuma huku ikionyesha kazi ya kila kamera kwenye simu hiyo.
Kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu simu hiyo ya Galaxy A9 (2018) yenye kamera nne kwa nyuma inakuja na kamera za Megapixel 8, Megapixel 10, Megapixel 24 pamoja na Megapixel 5, Kamera ya kwanza yenye megapixel 8 yenyewe inatumika kuchukua picha kwa upana, kamera ya pili yenye megapixel 10 hii ni Telephoto na kamera yenye Megapixel 24 hii ndio kamera ya kawaida na kamera ya mwisho ya megapixel 5 hii ni depth ambayo inachukua picha vizuri hasa wakati wa usiku. Kama unataka kujua sifa kamili za Galaxy A9 (2018) soma zaidi hapa.
Mpangilio wa kamera hizi unafanya simu hii pengine kuwa simu bora kwenye kupiga picha pengine kuliko simu nyingine za Samsung ambazo zimewahi kutoka hadi sasa. Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu sifa za simu hii ila endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza yote ya muhimu kuhusu simu hii mpya.