Wakati bado tukisubiri kiwanda cha simu kinacho tegemewa kujengwa na serikali huko Zanzibar, Huku bara mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya IPP hivi leo amezindua kampuni mpya ya IPP TouchMate ambayo itakuwa ikijihusisha na utengenezaji mbalimbali wa vifaa vya kielektroniki kama vile simu za mkononi, tablet, saa janja, pamoja na laptop.
Kampuni hiyo ya IPP TouchMate inategemewa kuajiri watu zaidi ya 2000 kwa awamu ya kwanza ambayo inategemewa kuanza miezi 3 ijayo. Mbali na hayo kwenye uzinduzi wa kampuni hiyo mkurugenzi huyo alizindua simu ya IPP TouchMate 4GX1 ambayo inasemekana kuwa simu ngumu zaidi na yenye kudumu na chaji zaidi hadi wiki moja.
Pia Mkurugenzi huyo amesema kuwa ajira kubwa zinategemewa kuwalenga walemavu ikiwa kama ni sehemu ya kutimiza ahadi yake aliyo itoa siku za karibuni.
baraka ,hongereni sana kwa hatua nzuri ya kuiwezesha tanznia ya viwanda, kanda ya ziwa kuna soko kubwa sana ya simu ,nadhani watu wa marketing tazameni kwa jicho la tatu ,nipo tayari kuwa miongoni wa kutengeneza soko huku kanda ya ziwa