Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Huu Ndio Ubora na Ugumu wa Simu Mpya ya iPhone Xs Max

Angalia hapa video ili kujua ubora na ugumu wa simu mpya ya iPhone Xs Max
Ugumu na ubora iPhone Xs Max Ugumu na ubora iPhone Xs Max

Kampuni ya Apple hivi karibuni imezindua simu zake mpya za iPhone za Mwaka 2018, Japo kuwa hizi ni simu mpya bado watu wengi wamekuwa wakitoa maoni mbalimbali huku wakidai kuwa msimu huu kampuni ya Apple imetoa simu zinazofanana huku zikiwa na tofauti kidogo sana…

Anyway hii ni mada ya siku nyingine kupitia uchambuzi, lakini kwa siku ya leo hebu tuangalie ubora na ugumu wa simu hizi mpya na zaidi simu ya iPhone Xs Max ambyo ndio simu ya bei ghali zaidi kwenye matoleo ya simu za mwaka huu.

Advertisement

Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii basi lazima utakuwa unamjua jerry, huyu ni mwana YouTube ambaye hufanya majaribio mbalimbali ya simu kuweza kujua ubora na ugumu wa simu pale tu zinapotoka rasmi. Sasa wiki hii jerry ameleta video mpya ambayo inaonyesha ubora na ugumu wa simu mpya ya iPhone Xs Max baada ya kuipitisha kwenye majaribio mbalimbali.

Kabla ujaweka majibu yako ni muhimu pia kuangalia video inayofuata ili kuweza kujua ubora na ugumu wa iPhone Xs Max ingawa sidhani kama hadi mwisho wa video hiyo bado dhumuni la mtu huyu ilikuwa ni kujaribuni ugumu na ubora wa simu hiyo…hebu niambie wewe unadhani hii ilikuwa ni test au ni uharibifu wa zaidi ya dollar $1000…

Mpaka hapo nadhani utakuwa umejua ugumu na ubora wa iPhone Xs Max, Kama unataka kujua ugumu na ubora wa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9 unaweza kusoma makala yetu iliyopita, pia unaweza kupata makala kama hizi kwa kutembelea Tanzania Tech kila siku pia usiache kupakua toleo jipya la App ya Tanzania Tech kupitia Play Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use