Tetesi : WhatsApp Kuja na Sehemu Mpya ya Dark Mode

Hivi karibuni utaweza kutumia app ya WhatsApp vizuri hasa wakati wa usiku
Sehemu ya WhatsApp Dark Mode Sehemu ya WhatsApp Dark Mode

WhatsApp ni moja kati ya application inayofanyiwa mabadiliko mengi sana siku hizi, lakini pamoja na kufanyiwa mabadiliko mengi ni kweli kwamba application hii haijawahi kubadilika muonekano wake kuanzia ilipotangazwa rasmi hapo mwaka 2009 hadi kufikia sasa.

Kwa mujibu wa tetesi, hayo yote yanaweza kubadilika kwani inasemekana hivi karibuni WhatsApp inaweza kuja na muonekano mpya kabisa ambao utafanya watumiaji kutumia App hiyo kwa urahisi zaidi hasa wakati wa usiku. Kama ilivyo sehemu ya Dark Theme kwenye tovuti ya YouTube, Dark Mode ni sehemu ambayo inatumika kuweka giza au rangi nyeusi kwenye programu fulani ili kukupa urahisi wa kuweza kusoma maandishi hasa wakati wa usiku, Hii husaidia kuweza kulinda macho yako na kuondoa madhara yanayotokana na kuangalia rangi nyeupe kwa muda mrefu.

Advertisement

Kwa mujibu wa tetesi kutoka tovuti ya WABetainfo, sehemu hiyo inaonekana kuwa iko kwenye hatua za awali na pengine hivi karibuni inaweza kuwafikia watumiaji mbalimbali wa programu ya WhatsApp ya mifumo yote ya iOS pamoja na Android.

Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi za lini sehemu hiyo inaweza kuja rasmi kwa watumiaji wote, lakini kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda sehemu hii basi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku na tutakuhabarisha pindi tu sehemu hii itakapo kuja rasmi kwenye app ya WhatsApp.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use