Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Xiaomi Mi 8 Pro na Mi 8 Lite

Kampuni ya Xiaomi imeongeza matoleo mpya ya simu za Xiaomi Mi 8
Sifa na bei ya Xiaomi Mi 8 Pro na Xiaomi Mi 8 Lite Sifa na bei ya Xiaomi Mi 8 Pro na Xiaomi Mi 8 Lite

Kampuni ya Xiaomi imeongeza familia ya Simu ya Xiaomi Mi 8 kwa kuja na simu mpya za Xiaomi Mi 8 Pro pamoja na Xiaomi Mi 8 Lite. Simu hizi mpya za Xiaomi zinakuja na maboresho mapya tofauti na simu ya Xiaomi Mi 8.

Tukianza na Xiaomi Mi 8 Pro inakuja na kioo cha inch 6.21 chenye resolution ya 1080x2248px huku kioo hicho kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya OLED display, simu hiyo pia inakuja na processor ya Snapdragon 845 chipset, ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 8.

Kwa upande wa Xiaomi Mi 8 Lite yenyewe inakuja na kioo cha inch 6.26 huku kioo chake kikiwa kimetengenzwa kwa teknolojia ya LCD, Vilevile simu hii ya Xiaomi 8 Lite inakuja na processor ya Snapdragon 660 chipset, ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 4. Simu hii pia inakuja na kamera mbili kwa nyuma huku kamera moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa na Megapixel 5, vilevile kwa mbele Mi 8 Lite ikiwa inakuja na kamera ya Selfie ya Megapixel 24. Sifa nyingine za Xiaomi Mi 8 Pro na Xiaomi Mi 8 Lite ni kama zifuatazo.

Advertisement

Sifa za Xiaomi Mi 8 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.21 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2248 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~402 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold na 4×1.8 GHz Kryo 385 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 lakini haina uwezo wa kuongezewa na memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20 yenye f/2.0, 0.9µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 1/2.55″, 1.4µm, 4-axis OIS, dual pixel PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.0, 1.12µm, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3000 mAh battery yenye teknolojia ya – Fast battery charging (Quick Charge 4.0+)
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black (inaonyesha mpaka ndani), Meteorite black na Shuguangjin.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Infrared face recognition, fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, barometer na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Xiaomi Mi 8 Pro inakuja na uwezo unaokaribiana na Mi 8 lakini kwenye upande wa Mi 8 Lite yenyewe inakuja na sifa za utofauti kidogo. Zifuatazo ndio sifa za Xiaomi Mi 8 Lite.

Sifa za Xiaomi Mi 8 Lite

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.26 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~403 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 na 4×1.8 GHz Kryo 260).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 512
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 128 lakini haina uwezo wa kuongezewa na memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.9, 1/2.55″, 1.4µm, dual pixel PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.0, 1.12µm, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3350 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging (Quick Charge 3.0)
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Twilight gold, Dream blue na Deep space gray.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint (rear-mounted), accelerometer, gyro, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Xiaomi Mi 8 Pro na Xiaomi Mi 8 Lite

Simu hizi zote zinatarajiwa kuingia sokoni kuanzia September 19 huku Xiaomi Mi 8 Pro yenye ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6 ikitarajiwa kuuzwa kwa Yuan ya China CNY 3,200 ambayo ni sawa na Tsh 1,070,000. Xiaomi Mi 8 Pro yenye GB 128 na RAM ya GB 8 yenyewe inatarajiwa kuuzwa kwa Yuan CNY 3,600 ambayo ni sawa na Tsh 1,201,000.

Kwa upande wa Xiaomi Mi 8 Lite yenyewe inatarajiwa kuuzwa kwa Yuan CNY 1,400 kwa toleo la simu hiyo lenye ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4 ambayo ni sawa na Tsh 467,000, uku toleo lenye GB 64 na RAM ya GB 6 likitarajiwa kuuzwa kwa Yuan CNY 1,700 sawa na Tsh 567,000 , uku pia toleo lenye GB 128 na RAM ya GB 6 likitarajiwa kuuzwa CNY 2,000 ambayo ni sawa na Tsh 667,000. Kumbuka bei zote ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo hivi bei inaweza kubadilika kutokana na viwango kubadilika pamoja na kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use