Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy J4 Plus na Galaxy J6 Plus

Zifahamu hizi hapa ndio sifa na bei ya Samsung Galaxy J4 Plus na Galaxy J6 Plus
Sifa na bei ya Samsung Galaxy J4+ na Galaxy J6+ Sifa na bei ya Samsung Galaxy J4+ na Galaxy J6+

Kampuni ya Samsung bado inaendelea kuzindua simu zake za mpya na hivi karibuni kampuni hiyo imezindua simu mpya za Samsung Galaxy J4+ pamoja na Galaxy J6+. Simu hizi zinakuja na muonekano mzuri pamoja na sifa nzuri kwa simu za bei nafuu.

Simu zote zinakuja na kioo cha inch 6.0 chenye resolution ya 720 x 1,480 pixel, vilevile simu zote mbili zinakuja na processor ya quad core processor yenye uwezo wa 1.4GHz. Mbali na hayo simu hizo mpya zinatofautiana kwenye upande wa RAM kwani Galaxy J6+ inakuja na RAM kwa machaguo mawili ya GB 3 na GB 4, wakati Galaxy J4+ inakuja na machaguo ya RAM kati ya GB 2 pamoja na GB 3. Sifa za Galaxy J6+ ni kama zifuatazo.

Advertisement

Sifa za Samsung Galaxy J6+

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1480 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~274 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm MSM8917 Snapdragon 425 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 308
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 32 na nyingine inayo GB 64 lakini haina uwezo wa kuongezewa na memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 3 na nyingine ikiwa na GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.9, 28mm, AF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Red na Grey.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Pembeni).

Kwa upande wa Galaxy J4+ yenyewe haina tofauti sana na Galaxy J6+ lakini tofauti kubwa iliyopo ni kwenye upande wa ukubwa wa ndani pamoja na RAM. Sifa za Galaxy J4+ ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy J4+

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1480 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~274 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm MSM8917 Snapdragon 425 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 308
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 16 na nyingine inayo GB 32 lakini haina uwezo wa kuongezewa na memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 2 na nyingine ikiwa na GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye f/1.9, 28mm, AF, huku zote ikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Red na Grey.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Pembeni).

Bei ya Samsung Galaxy J6+ na Galaxy J4+

Kwa upande wa bei simu hizi mpya bado haijajulikana rasmi ila inasemekana kuwa Galaxy J4+ inakadiriwa kuuzwa kwa Euro 190 ambayo ni sawa na Tsh 506,000 bila kodi. Kwa upande wa Galaxy J6+ yenyewe inakadiriwa kuuzwa kwa Euro 240 ambayo ni sawa na Tsh 639,000. Kumbuka bei hizi zinatofautiana kulingana na ukuwa wa ndani wa simu husika pia bei inaweza kubadilika kulingana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use