in

Motorola Yazindua Simu Mpya ya Motorola One Power (P30 Note)

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya Motorola One Power

Sifa na Bei ya Motorola One Power (P30 Note)

Kampuni ya Motorola hivi karibuni imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Motorola One Power au P30 Note huko nchini India, simu hii inakuja na muonekano unaofanana sana na iPhone X huku ikiwa na ukingo wa juu maarufu kama top notch tofauti na simu nyingi kutoka kampuni hiyo.

Motorola One Power au (P30 Note) inakuja na Battery kubwa ya 5000mAh ambayo kwa mujibu wa kampuni hiyo inaweza kudumu na chaji kwa muda wa siku mbili kwa kuchaji mara moja tu, vilevile motorola inadai kuwa simu hii pia inaweza kudumu na chaji kwa muda wa siku moja na masaa kadhaa iwapo utakuwa unacheza game mfululizo kwenye simu hiyo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Mbali na battery ambayo ndio maboresho makubwa ya simu hii, Motorola One Power (P30 Note) inakuja na kioo cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS display ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2246 pixels pamoja na uwiano wa 18.7:9 ratio.

Simu hii pia inakuja na mfumo wa Android 8.1 ambao unaweza ku-update hadi kwenye mfumo mpya wa Android 9 Pie. Simu hii inatumia processor ya Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 3, GB 4 na GB 6. Motorola One Power inakuja na kamera mbili za nyuma ambapo kamera moja inakuja na uwezo wa Megapixel 16 na nyingine inakuja na uwezo wa Megapixel 5. Sifa nyingine za Motorola One Power ni kama zifuatazo.

Sifa za Motorola One Power

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.21 chenye teknolojia ya IPS LCS capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2246 pixels, na uwiano wa 18.7:9 ratio (~402 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) inaweza ku-update hadi Android 9 Pie
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Kryo 260.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 509.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 32 na nyingine inakuja na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu tatu moja ikiwa na RAM ya GB 3 na nyingine ikiwa na GB 4 na ya mwisho ikiwa na GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 12 yenye f/2.0, 1.25µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.8, 1.12µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye ff/2.2, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 5000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging (15W)
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa moja ya Midnight Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Motorola One Power

Kwa upande wa bei, simu hii imetangazwa hivi leo kuanza kupatikana huku inchini India ambapo itakuwa inaanzia kuuzwa kwa rupee ya india Rs 15,999 ambayo ni sawa na Tsh 503,000 bila kodi. Bado hakuna taarifa zaidi kuhusu ujio wa simu hii kwenye nchi nyingine mbalimbali hivyo endelea Kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi kuhusu simu hii.

Motorola Yazindua Simu Mpya ya Motorola One Power (P30 Note)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.