Kama umekuwa mfuatiliaji wa maswala mazima ya teknolojia najua utakuwa unajua kuwa kampuni ya Apple hapo jana ilizindua simu zake mpya za iPhone Xs, iPhone Xs Max pamoja na iPhone XR. Kama unataka kujua sifa kamili, muonekano na bei ya iPhone Xs na iPhone Xs Max unaweza kusoma makala yetu nyingine iliyopita na utaweza kujua yote ya muhimu kuhusu simu hizo.
Kwa sasa hebu tuangalie sifa za iPhone XR, kwa upande wa simu ya iPhone XR, yenyewe inakuja na kioo cha IPS LCD cha inch 6.1 ambacho pia kinakuja na resolution ya 828 x 1792 pixels kioo ambacho pia kinauwezo wa kuonyesha rangi milioni 16, Japo kuwa kioo hicho cha LCD hakionyeshi kwa ubora kama ilivyo kwenye simu za iPhone Xs na Xs Max lakini ni wazi kuwa bado simu hii imeweza kujitahidi sana kuonyesha rangi bora.
Mbali na hayo simu hii inakuja na processor ya Hexa-core ambayo inaendeshwa na chipset mpya kutoka Apple ya A12 Bionic ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3, Kama zilivyo simu za iPhone Xs na Xs Max simu hii pia inakuja na kamera ya megapixel 12 lakini utofauti uliopo ni kuwa iPhone XR inakuja na kamera moja kwa nyuma, Sifa nyingine za iPhone XR ni kama zifuatazo.
Sifa za iPhone XR
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.1 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 828 x 1792 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~326 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12
- Uwezo wa Processor – Hexa-core.
- Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12 Bionic Chipset.
- Uwezo wa GPU – Apple GPU (4-core graphics).
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 nyingine GB 128, na nyingine GB 256 zote zikiwa hazina uwezo wa memory card.
- Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 3.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@60fps.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 12 yenye f/1.8, 28mm, 1.4µm, OIS, PDAF.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion (ukubwa wa battery haujajulikana) battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS. USB ya Type-C 2.0, proprietary reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tano za Black, Red, Yellow, Blue na Coral
- Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP67 dust/water proof (maji ya urefu wa 1m kwa dakika 30), pia Inakuja na Apple Pay.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Haina Fingerprint, inakuja na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Face ID).
Bei ya iPhone XR
Kwa upande wa bei ya iPhone XR, Simu hii itauzwa kwa dollar za marekani $749 ambayo ni swa na Tsh 1,712,000 kwa toleo la iphone ya GB 64, toleo la GB 128 litakuwa likianzia dollar $799 ambayo ni sawa na Tsh 1,827,000 bila kodi na toleo la mwisho la GB 256 litauzwa kwa dollar $899 ambayo ni sawa na Tsh 2,055,000 bila kodi. Upatikanaji wa simu hii utaanza rasmi kuanzia tarehe 19 ya mwezi ujao (October).