Hatimaye Samsung Yazindua Tablet Mpya ya Galaxy Tab S4

Hizi hapa sifa na bei ya tablet mpya ya Galaxy Tab S4
Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Tab S4 Pic 2 Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Tab S4 Pic 2

Baada ya tetesi za ujio wa tablet mpya ya Galaxy Tab S4, hatimaye leo kampuni ya Samsung imezindua tablet hiyo rasmi na ukweli tablet hii ina mabadiliko mengi makubwa ukilinganisha na tablet ya mwaka jana (2017) ya Galaxy Tab S3.

Galaxy Tab S4 inakuja na maboresho kama vile kioo kikubwa cha inch 10.5 tofauti na tableti ya mwaka jana ambayo yenyewe ilikuwa na kioo cha inch 9.7. Mbali na hayo tablet hii inakuja na ukingo mdogo sana hivyo kufanya kioo cha tab hiyo kuonekana kikubwa zaidi. Vilevile Tab hii ni tab ya kwanza kutoka samsung kuwa na teknolojia ya Iris Scanner, teknolojia mbayo inaongeza ulinzi kwenye tab yako kwa kuwezesha kufungua tab hiyo kwa kutambua masho pamoja na uso.

https://youtu.be/ufAuTtB5mV4

Advertisement

Mbali na hayo yote tablet hii ya Galaxy Tab S4, inakuja na keyboard maalum ambayo unaweza kuitumia ili kubadilisha matumizi ya tablet hiyo kuwa kama kompyuta mpakato au Laptop. Vilevie tukibakia hapo hapo kwenye uwezo wa kubadilisha tab hiyo kuwa laptop.. Galaxy Tab S4 inakuja na teknolojia ya Samsung DeX ambayo hii inafanya uweze kutumia tablet hiyo kwenye kompyuta huku ukiwa unaweza kutumia Mouse pamoja na keyboard, kama inavyo kuwa kwenye kompyuta ya kawaida.

Zaidi ya yote tablet hii inakuja na kalamu maalum ambayo unaweza kutumia kuandika au kuchora kwa kutumia programu maalum iliyoko ndani ya Tablet hiyo. Mengine kuhusu tablet hii, inakuja processor ya Snapdragon 835 chipset yenye kusaidiwa na RAM ya GB 4 na ukubwa wa ndani wa GB 64 au GB 256 ambayo inaweza kuongezewa na memory kadi ya GB 400. Sifa nyingine za Tablet hii ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy Tab S4

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 10.5 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1600 x 2560 pixels, 16:10 ratio (~287 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.35 GHz Kryo & 4×1.9 GHz Kryo), Qualcomm MSM8998 Snapdragon 835 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 540
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko tablet mbili moja ikiwa na GB 64 na nyingine GB 256 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye 1080p@30fps
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye AF, pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 7300 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, USB 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; magnetic connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na White
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Ipo inayotumia laina na ipo ambayo Haitumi Laini (Inatumia Wi-Fi), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint, Iris Scanner (Kufungua kwa Kutambua,Macho na Uso).

Bei ya Samsung Galaxy Tab S4

Kwa upande wa bei Galaxy Tab S4, itauzwa kwanza kwa nchini marekani kuanzia tarehe 10 mwezi huu kupitia tovuti za Amazon, Best Buy, pamoja na Samsung Store. Galaxy Tab S4 itauzwa kwa dollar za marekani $649.99 sawa na Tsh 1,483,000 bila kodi kwa tablet inayotumia Wi-Fi, Huku dollar $850 sawa na Tsh 1,939,000 bila kodi kwa tablet inayotumia LTE.

Kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use