Hivi karibuni kampuni ya Infinix imezindua simu mpya ya Infinix Hot S3X, simu hii ni toleo jipya la maboresho la simu ya Infinix Hot S3 ambayo ilizinduliwa mapema mwaka huu. Infinix Hot S3X ni simu ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya Infinix ambayo inakuja na ukingo wa juu maarufu kama top notch, mbali na hayo simu hii inakuja na muonekano kama iPhone X, pengine labda ndio chanzo cha kuitwa Hot S3X.
Infinix Hot S3X inakuja na kioo cha inch 6.2 ambacho kimetengenezwa kwa LCD ambayo kina resolution ya 720 x 1500 pixels. Simu hii pia inakuja na RAM ya GB 3 au GB 4 ambayo inasaidiwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 430 yenye uwezo wa 64-bit Octa-core 1.4 GHz Cortex-A53. Hot S3X inakuja na GPU ya Adreno 505.
Simu hii pia inakuja na kamera mbili kwa nyuma zenye uwezo wa Megapixel 13 na Megapixel 2 huku kamera ya mbele yenyewe inakuja na uwezo wa Megapixel 16. Sifa nyingine za Infinix Hot S3X ni kama zifuatazo.
Sifa za Infinix Hot S3X
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.2 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~268 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – 1.4GHz Octa-Core.
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm Snapdragon 430 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Adreno 505.
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ina RAM ya GB 3 na nyingine ina RAM ya GB 4.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye LED Flash.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine inakuja na Megapixel 2 zenye Autofocus na Flash ya Dual-LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-ion 4000 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue, na Gray
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM,), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Light Sensor, G-sensor, E-compass, Proximity Sensor, Face ID Sensor, Fingerprint.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso (Face ID)
Bei ya Infinix Hot S3X
Kuhusu bei bado simu inategemewa kuuzwa kwa makadirio ya shilingi za kitanzania kuanzia Tsh 350,000 hadi Tsh 400,000. Vilevile tegemea kuipata simu hii kupitia soko la Jumia, hivyo pale itakapo tangazwa rasmi nitakuwekea link hapa kwaajili ya wewe kuipata kwa urahisi.
Basi hizo ndio sifa na bei ya simu mpya ya Infinix Hot S3X, kama una maoni yoyote au maswali usiache kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.
wadau samahani sana kwa usumbufu langu nikutaka kujua ifinix zero4 plus na oppo R9M ipi bora ikiwa pamoja processer zake
hii infinix s3x imeshatoka au bado
tayari ila inawezekana bado haijafika hapa Tanzania.
hii infinix s3x imeshatoka
Nimeipenda hiyo
ni nzur kwakweli
Maduka yenu yako wapi kwa dar_es_salaam
Jaman mm naitaka hii simu anytime kama vipo
Jaman mm naitaka hii simu anytime kama vipo
Simu infinix hot S3 xos honeybee dukani kwa bei ya reja reja ni tsh. ngapi
mimi nimeikuta dukani ikiuzwa tsh.585000. Nikaomba kupunguziwa wakagomea kwenye tsh. 45000. Je, ndio bei yake halali?