in

Sifa na Bei ya BlackBerry Evolve na BlackBerry Evolve X

Zifahamu kwa undani hizi hapa sifa za BlackBerry Evolve na Evolve X

Sifa na Bei ya BlackBerry Evolve na BlackBerry Evolve X

Baada ya kampuni ya BlackBerry kuzindua simu yake mpya ya BlackBerry Key2 miezi miwili iliyopita, hivi leo kampuni hiyo imerudi tena na simu zake mpya mbili za BlackBerry Evolve na BlackBerry Evolve X.

Simu hizi zinakuja na muonekano wa tofauti na muonekano uliozoeleka kwenye simu za Blackberry kwani sasa simu hizi zinakuja na kioo kizima bila kuwa na keyboard ambayo tumezoea kuona kwenye simu nyingi za Blackberry.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Tukianza kuangalia kwa upande wa simu ya Blackberry Evolve, simu hii inakuja na RAM ya GB 4 ambayo iko sambamba na processor ya Snapdragon 450 chipset yenye speed ya 1.8 GHz, Ukubwa wa ndani wa simu hii ni GB 64 ambayo inaweza kuongezewa na memory card hadi ya GB 256, sifa nyingine za BlackBerry Evolve ni kama zifuatazo.

Sifa za BlackBerry Evolve

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.99 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~403 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53, Qualcomm SDM450 Snapdragon 450 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 506
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 16 yenye LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 yenye uwezo wa (1/3.1″, 1.12µm, PDAF) na nyingine ikiwa na Megapixel 13 yenye (1/3.1″, 1.12µm, PDAF), huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, 3.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Kwa upande wa BlackBerry Evolve X yenyewe inakuja na processor ya Snapdragon 660 chipset yenye speed ya 2.2 GHz ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa ndani wa GB 64 ambao unaongezewa na memory card hadi ya GB 256. Sifa nyingine za BlackBerry Evolve X ni kama zifuatazo.

Sifa za BlackBerry Evolve X

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.99 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~403 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260), Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 512.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 16 yenye LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye uwezo wa (f/1.8, 1/2.8″, 1.29µm, PDAF) na nyingine ikiwa na Megapixel 13 yenye (f/2.6, 1/3.4″, 1.0µm, PDAF), huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, 3.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya BlackBerry Evolve na BlackBerry Evolve X 

Kwa upande wa bei ya simu hizi BlackBerry Evolve na BB Evolve X, BlackBerry Evolve itauzwa kwa dollar za marekani $365 sawa na Tsh 833,000. Kwa upande wa BlackBerry Evolve X yenyewe itauzwa kwa dollar za marekani $510 sawa na Tsh 1,164,000. Simu hizi zitakuwa sokoni kuanzia katikati ya mwezi huu september mwaka 2018.

Sifa na Bei ya BlackBerry Evolve na BlackBerry Evolve X
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.