Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Dalili 10 Zinazoonyesha Simu Yako Imedukuliwa (Hacked)

Hizi hapa ndio baadhi ya dalili simu yako imekuwa hacked
simu imedukuliwa imekuwa hacked simu imedukuliwa imekuwa hacked

Kama ulikuwa unadhani kwa sababu uko na simu yako kila mara basi haiwezi kudukuliwa au kuwa hacked basi umekosea, Mara nyingi wadukuaji wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kuweza kudukua simu mbalimbali bila hata wewe kujua. Sasa leo hapa Tanzania Tech tumekuandalia dalili 10 ambazo unaweza kuziona endapo simu yako imedukuliwa (imekuwa Hacked)

Dalili hizi zitakusaidia wewe kuweza kujua hata kama kuna mtu anasoma meseji zako kabla ya wewe hujaziona, vilevile utaweza kujua njia za kuweza kujilinda na udukuaji wa aina hii pamoja na hatua za kufuata kama simu yako imeduliwa, basi bila kupoteza muda let’s get to it…

Advertisement

1. Unakuta App Mpya kwenye Simu yako Ambazo Hukuziweka Wewe

Kama umekuwa ukikutana na apps mbalimbali kwenye simu yako ambazo hujaziweka wewe basi ni vyema kuchukua hatua za haraka. Mara nyingi kama mtu anataka ku-hack simu yako ni lazima anatakiwa kupata data za muhimu za simu yako, hivyo njia mojawapo ya kuweza kupata data hizo ni kwa kupitia njia ya kuinstall app kwenye simu yako. Kampuni za utengenezaji wa simu zinapenda kuweka app zao pale unapo nunua simu, hivyo hakikisha kama app hizo ni za kampuni husika kwa kutafuta jina la App kupitia Google.

2. App Hazifanyi Kazi Kama Inavyotakiwa au Kama Hapo Awali

Kama kwa namna moja ama nyingine app mpya unazoweka kwenye simu yako zinafanya vizuri na App ambazo zilikwepo kwenye simu yako hazifanyi kazi vizuri basi hiyo ni dalili huwenda simu yako imeadhiriwa na Malware.

3. Simu Yako Inaanza Tabia ya Kuisha Chaji Ghafla

Kama simu yako ilikuwa inadumu na chaji lakini ghafla inaonyesha inaisha chaji kwa haraka sana basi hiyo ni dalili kuna mtu anadukua simu yako. Mara nyingi hii inasababishwa na app mpya ambazo hazikwepo awali ambazo zinafanyakazi ndani ya simu yako bila hata wewe kuzitumia.

4. Simu Yako Inaanza kuwa Slow Sana au Taratibu

Kama simu yako ilikuwa inafanya kazi kwa haraka na ghafla unaanza kuona inakuwa slow basi hiyo ni dalili simu yako imedukuliwa. Kama ilivyo kwenye chaji, hii pia usababishwa na app mpya ambazo zinafanya kazi nyuma ya pazia hata kama wewe huzitumii app hizo.

5. Simu Yako Inakuwa ya Moto Hata Kama Huitumii

Kuna sababu nyingi zinazo sababisha simu kuwa ya moto, lakini kama kwa namna yoyote hutumii simu yako au simu yako haifanyi kazi yoyote basi hiyo ni ishara simu yako imedukuliwa. Hii pia inaweza kusababishwa na baadhi ya programu ambazo zinafanya kazi nyuma ya pazia hata kama huzitumi.

6. Simu Yako Inajizima na Kujiwasha Mara kwa Mara

Kama simu yako inatatizo kwenye mfumo wa uendeshaji basi hii inaweza kutokea kutokana na hilo. Lakini kama unahakika simu yako ni mpya na kwa namna yoyote hujawai kuiharibu kwa kuangusha au vinginevyo basi hii ni ishara kuwa simu yako imedukuliwa.

7. Simu Yako Inakuwa Ngumu Kuzimika

Again.. Kama una hakika simu yako haijawahi kupata tatizo lolote la kuangushwa, kufunguliwa au ubovu wa namna yoyote, na kila unapotaka kuzima simu yako inakuwa ngumu kuzima basi hii ni wazi kabisa hii ni dalili ya simu yako kudukuliwa.

8. Unasikia Mwangwi Unapo Piga au Kupokea Simu

Kama kwa namna yoyote una hakika simu yako ni nzima na kila unapo pigiwa au kupokea simu unasikia mwangwi kwenye simu yako basi ni vyema kuchukua hatua za mapema kwani hii ni dalili kuna mtu amedukua simu yako na anasikiliza maongezi yako.

9. Simu Yako Inatumia Bando (Internet) Sana Kuliko Awali

Kama unaona tatizo la simu yako kumaliza data hata kama hujazitumia na kama unaona mabadiliko makubwa ya data kwenye matumizi yako ya kawaida ya Internet basi hii ni wazi kuwa simu yako imedukuliwa. Kama baadhi ya sababu hapo juu, mara nyingi wadukuaji huweza kupata data za muhimu za simu yako kupitia app mbalimbali na ili app hizo ziweze kufanya kazi zinahitaji internet sasa kama ulikuwa unaweza kudumu na GB 1 kwa siku na sasa GB 1 haimalizi hata masaa 5 basi hii ni wazi kuwa simu yako imedukuliwa.

10. Huwezi Kupiga Simu au Inakatika Hata Kama Unaela Kwenye Simu

Mara nyingi tatizo hili hutokea endapo kuna tatizo la kimtandao, Kama unapata atatizo kama hili mara kwa mara na unaona watu wengine wa mtandao kama wako wanaweza kupiga simu basi hii ni dalili simu yako imedukuliwa.

Na hizo ndio baadhi tu ya dalili ambazo zinaweza kuonyesha kama simu yako imekuwa hacked, kama unaona dalili hizi mara kwa mara kwenye simu yako basi ni muhimu kufuata hatua hapo chini ili kuhakikisha unarudisha simu yako kwenye hali ya kawaida ili kuwendelea kutumia simu yako ikiwa salama

Njia za Kufuata kama Simu Yako Imedukuliwa

  • Hakikisha kama uliweka App fulani kwenye simu yako ndipo ukaanza kuona dalili hizi basi hakikisha una uninstall au unaondoa app hiyo kwenye simu yako haraka.
  • Hakikisha unaweka programu za kuangalia simu yako kama ina virusi, hapa pia kuwa makini kwani programu zingine za aina hiyo zinashutumiwa kuharibu simu badala ya kurekebisha. Unaweza kutumia App ya Kaspersky Mobile Antivirus kwa ulinzi zaidi, unaweza kuipakua mwisho wa makala hii.
  • Kama unapata dalili hizi na njia zote hapo juu hazijaweza kukusaidia basi ni wakati wa kuchukua hatua ya kuweza kufanya RESET ya simu yako. Hakikisha vitu unavyo viitaji unaviweka pembeni lakini pia hakikisha vitu hivyo vinachunguzwa kwanza na programu za kuangalia virusi kabla hujarudisha vitu hivyo kwenye simu yako.

Sasa kama umefuata njia zote hizo na unaona bado simu yako inaonyesha dalili hizo basi ni muhimu kuwasiliana na huduma ya wateja kwa kampuni ulio nunulia simu yako.

Lakini pia kinga ni bora kuliko tiba, haya hapa ni baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafuata ili kuhakikisha unajilinda na watu wabaya wanaotaka kudukua simu yako.

Njia za Kufuata ili Kuzuia Simu Yako Kudukuliwa

  • Hakikisha Una install app ambazo unaziamini kwenye simu yako au app ambazo unauhakika na chanzo cha app hizi.
  • Hakikisha una acha tabia ya kubofya link zinazotumwa na watu ambao huwaju kwenye sehemu ya meseji.
  • Hakikisha unakuwa na password kwenye simu yako au programu inayoweza kuzuia app kufanya kazi mpaka utakapo weka password.
  • Hakikisha unachagua sehemu ya Charge only pale unapochaji simu yako kwenye kompyuta ambayo sio yako au ambayo inamilikiwa na mtu ambae humuamini.
  • Mara nyingi usichague sehemu ile inayo uliza REMEMBER PASSWORD badala yake tumia programu za kuaminika za kuweza kutunza password zako ili uweze kukumbuka kwa urahisi. Moja ya programu hizo unaweza kupakua link iko hapo chini mwisho wa makala hii.
  • Hakikisha huunganishi Wi-Fi za bure za sehemu ambazo huzijui au hakikisha unaondoa sehemu ya Automatic Connection kama unatumia Wi-Fi za sehemu kama hoteli au migahawa.
  • Pia Hakikisha una achana na tabia ya kutumia Wi-Fi za bure hasa zile zenye majina kama Free Wi-Fi au Wi-Fi Bure au majina mengine yenye lengo la kukuvutia.
  • Zima Bluetooth na Wi-Fi pale unapo maliza kutumia hakikisha Wi-Fi yako inayo password hasa kama unatumia sehemu ya Hotspot.

Na hizo ndio baadhi tu ya njia ambazo unaweza kuzifuata ili kuweza kujilinda ili mtu yoyote asiweze kuhack simu yako. Kumbuka inawezekana pia wadukuaji wanazijua njia hizi za kujilinda hivyo ni muhimu kuwa makini zaidi kwani hiyo ndio njia pekee ya kuweza kujilinda zaidi na kuzuia mtu asiweze ku-hack simu yako. Unaweza kupata app tulizo ongelea kupitia makala hii hapo chini.

Kaspersky Mobile Antivirus – Android

Kaspersky Security Cloud – iOS

Dashlane Free Password Manager – Android

LastPass Password Manager – Android

Kama kuna mahali unahisi hujaelewa au kama una swali unaweza kuuliza swali lako HAPA, pia unaweza kuuliza swali lako kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa maujanja zaidi kama haya hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

4 comments
  1. kuna njia ambayo imekuwa ikitajwa kuwa ukiandika kwenye simu inakuonesha kama siku yako inadukuliwa. Ni ipi hiyo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use