WhatsApp Yaongeza Sheria Mpya Kuzuia Habari za Kuzusha

Idadi ya meseji unazo forward kupitia App ya WhatsApp sasa imepunguzwa
sheria mpya whatsapp sheria mpya whatsapp

Habari za kuzusha au habari za uongo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ni moja kati ya matatizo ya nchi nyingi sana kwa sasa ikiwemo Tanzania. Sasa ili kupambana na habari hizi, Facebook kupitia app yake ya WhatsApp sasa imeanza kuleta sheria mpya za utumiaji wa programu ya WhatsApp sheria ambazo zitapunguza usambaaji wa habari hizo kwa kiwango fulani.

Kwa mujibu wa habari kupitia blog ya WhatsApp, hivi karibuni watumiaji wa programu ya WhatsApp wataanza kuwekewa vikwazo kwenye idadi ya meseji wanazo (forward) kwa watu wengine pamoja na magroup mbalimbali. Kwa mujibu wa habari hiyo, sasa watumiaji wa programu hii wataweza ku-forward meseji hadi kwa watu 20 pekee, huku nchi nyingine kama India watumiaji wanaruhusiwa ku-forward meseji hadi kwa watu watano 5 pekee.

Hata hivyo WhatsApp imeandika kuwa, Kusambaa kwa habari za uzushi imekuwa ni tatizo kubwa sana hasa kwa watumiaji wa programu hiyo wa nchini India, ambapo pia kuna watumiaji wengi wa programu hiyo takribani milioni 200, huku nchi hiyo ikiongoza kwa usambazaji wa habari za kuzusha ikifuatiwa na nchi ya Brazili.

Advertisement

Kwa sasa watumiaji wote wa WhatsApp wataweza ku-forward meseji hadi kwa watu 20 au magroup 20, huku jitihada nyingine ya kupambana na habari za kuzusha zikiwa ni kuonyesha kama meseji imetoka kwa mtu mwingine kwa kuwekewa alama ya (Forwarded) juu ya meseji hiyo.

WhatsApp imeandika inaendelea na jitihada za kupambana na habari za uongo au za kuzusha, na itaendelea kuleta sheria mpya kwa watumiaji wa nchi zinazotumia programu hiyo kusambaza habari za uongo au habari za kuzusha.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use