Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Xiaomi Yazindua Simu Mpya za Xiaomi Mi A2 na Mi A2 Lite

Zifahamu kwa undani hizi hapa sifa za Xiaomi Mi A2 na Mi A2 Lite
Xiaomi Mi A2 Lite Xiaomi Mi A2 Lite
Xiaomi Mi A2 Lite

Hivi leo huko nchini Spain kwenye mji wa Madrid, kampuni ya Xiaomi imefanya uzinduzi wa simu zake mpya za Xiaomi Mi A2 na Mi A2 Lite, simu hizi ni matoleo mapya ya simu za Xiaomi Mi A1 simu zilizo zinduliwa rasmi hapo mwaka jana 2017.

Mbali ya kuwa simu hizi ni maboresho ya simu zilizopita za Xiaomi Mi A1, lakini pia simu hizi zinakuja na sehemu mpya mbalimbali ikiwa pamoja na mfumo wa Android One. Kwa upande wa Xiaomi Mi A2 inakuja na kioo cha inch 5.99 IPS LCD chenye resolution ya 1080 x 2160 pixel ambacho pia kina ulinzi wa Gorilla Glass 5.

Advertisement

Simu hii pia inakuja na kamera nzuri ya Megapixel 20 kwa mbele yenye teknolojia ya AI pamoja na sehemu ya LED Flash kwaajili ya kupiga picha zako za Selfie hata wakati wa usiku. Kwa nyuma simu hii ya Xiaomi Mi A2 inakuja na kamera mbili za Megapixel 12 pamoja na Megapixel 20 ambazo nazo zinakuja na teknolojia ya AI au Artificial intelligence. Sifa nyingine za Xiaomi Mi A2 ni kama zifuatazo.

Sifa za Xiaomi Mi A2

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.99 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~403 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo); Android One
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 na 4×1.8 GHz Kryo 260), Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 512
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu tatu moja ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 32, nyingine GB 64 na ya mwisho inakuja na GB 128 zote zikiwa Hazina sehemu ya memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko RAM za aina mbili GB 4 pamoja na GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 24 yenye f/2.2, 1/2.8″, 1.0µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye (f/1.8 1/2.9″, 1.25µm) na nyingine ikiwa na Megapixel 20 yenye f/1.8, 1/2.8″, 1.0µm na PDAF. Kamera zote mbili zinasaidiwa na flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 5V/2A (Quick Charge 3.0).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tano za Black, Gold, Blue, Red na Rose Gold.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint (Kwa Nyuma).

Kwa upande wa simu ya Xiaomi Mi A2 Lite, yenyewe inakuja ikiwa na kioo cha inch 5.88 chenye resolution ya 1080 x 2280 pixels pamoja na aspect ratio ya 19:99, pia simu hii inakuja na ukingo wa juu maarufu kama top notch.

Vilevile simu hii inakuja na kamera mbili kwa nyuma, moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa na Megapixel 5. Xiaomi Mi A2 Lite inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 12 ambayo inakuja na teknolojia za phase detection autofocus, sifa nyingine za Xiaomi Mi A2 Lite ni kama zifuatazo.

Sifa za Xiaomi Mi A2 Lite

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.84 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, 19:9 ratio (~432 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo); Android One
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53, Qualcomm MSM8953 Snapdragon 625 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 506
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 32, nyingine GB 64 zote zikiwa zinauwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko RAM za aina mbili GB 3 pamoja na GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 5 yenye f/2.0.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 5 yenye (f/2.2, 1.12 μm, depth sensor) na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.2, 1.25 μm, na PDAF. Kamera zote mbili zinasaidiwa na flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, micro USB 2.0.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tano za Black, Blue, Gold ambazo zitapatina nchi zote, huku rangi za Rose Gold na Red zitapatikana kwa nchini china pekee..
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Xiaomi Mi A2 na Xiaomi Mi A2 Lite

Kwa upande wa bei ya simu hizi za Xiaomi Mi A2 yenyewe inakuja na matoleo matatu tofauti, toleo kwanza lenye ukubwa wa ndani wa GB 32 na RAM ya GB 4 litauzwa kwa Euro €250 sawa na Tsh 667,000. Huku toleo la Mi A2 ya ukubwa wa ndani wa GB 64 na RAM ya GB 64 ikiwa ni Euro €280 sawa na Tsh 747,000 na toleo la mwisho la Xiaomi Mi A2 lenye ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6 likiwa kwa Euro €350 sawa na Tsh 933,000.

Kwa upande wa Xiaomi Mi A2 Lite yenyewe inakuja kwa matoleo mawili, huku toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 32 na RAM ya GB 3 likiwa linauzwa kwa Euro €180 sawa na Tsh 480,000 huku toleo la pili lenye ukubwa wa ndani wa GB 64 na RAM ya GB 4 likiwa linauzwa kwa Euro €230 sawa na Tsh 614,000. Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Simu zote hizi zitaanza kupatikana rasmi kuanzia mwezi ujao August 10, kupitia nchi mbalimbali barani Ulaya, Asia Pasifiki, Mashariki ya Kati na Afrika, pamoja na barani Amerika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use