Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy On6

Zihamu kwa undani sifa na bei ya simu mpya ya Galaxy On6
Sifa na Bei ya Galaxy On6 Sifa na Bei ya Galaxy On6

Kampuni ya Samsung bado inaendelea na kuzindua simu zake mpya mwaka huu 2018, na kabla ya kuzinduliwa kwa Simu mpya ya Galaxy Note 9, Samsung imerudi tena na mfululizo wa simu mpya ya Galaxy On6 ambayo kwa mwaka huu imefanyiwa maboresho zaidi.

Kwa muonekano wa sifa, simu hii inafanana kabisa na simu mpya ya Galaxy J6 (2018) ambayo imezinduliwa hivi karibuni na kampuni ya Samsung, Simu hii ya Galaxy On6 inakuja na kioo cha Inch 5.6 chenye teknolojia ya Super AMOLED pamoja na resulution ya 1480x720px na Aspect Ratio ya 18.5:9.

Advertisement

Upande wa processor simu hii inakuja na processor ya Exynos 7870 chipset ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64 yenye uwezo wa kuongezewa kwa kutumia memory card, sifa nyingine za Samsung Galaxy On6 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy On6

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.6 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1480×720 pixels, 18.5:9 ratio.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.6GHz, Exynos 7870 chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 520 (bado haina uhakika)
  • Ukubwa wa Ndani –  GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 16 yenye autofocus, dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Blue na Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa kutambua uso (Face ID) Pia inayo Fingerprint (Kwa nyuma)

Bei ya Samsung Galaxy On6

Simu hii kwa sasa imezinduliwa kwa nchini India na huko inapatikana kwa Rupia ya India INR 14,490 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 480,000. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa hapa Tanzania kutokana na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Na hizo ndio sifa pamoja na bei ya simu mpya ya Galaxy On6 ambayo imezinduliwa siku ya leo huko nchini India. Nini maoni yako unaonaje simu hii mpya kutoka Samsung..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use