Baada ya kushindwa kuzindua simu hii ya Nokia X5 au Nokia 5.1 Plus siku ya tarehe 11, hatimaye kampuni ya Nokia hivi leo imezindua simu iyo mpya ya Nokia X5 ambayo inakuja na muonekano mzuri pamoja na sifa nzuri. Nokia X5 ni moja kati ya simu bora za Nokia kwa mwaka huu 2018.
Nokia X5 inakuja na kioo cha inch 5.86 chenye teknolojia ya IPS LCD chenye resolution ya 720 x 1520 pixel pamoja na aspect ratio au uwiano wa 19:9. Kwa upande wa processor simu hii ya Nokia X5 inakuja na processor ya MediaTek Helio P60 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 kwa simu yenye ukubwa wa ndani wa GB 32 na nyingine ikiwa na RAM ya GB 4 kwa simu yenye ukubwa wa GB 64.
Kwa upande wa nyuma, Nokia X5 inakuja na sehemu ya Fingerprint pamoja na kamera mbili ambazo zinauwezo wa Megapixel 13 na megapixel 5. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera yenye uwezo wa Megapixel 8 yenye teknolojia ya AI portraits na beauty mode, sifa nyingine za Nokia 5X au Nokia 5.1 Plus ni kama zifuatazo.
Sifa za Nokia X5 au Nokia 5.1 Plus
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.86 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2244 pixels, 19:9 ratio.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android One 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53, MediaTek’s Helio P60 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Bado Haijajulikana
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja ikiwa na GB 32 na nyingine ikiwa na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
- Ukubwa wa RAM – GB 3 na GB 4
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 5. Kamera zote mbili zinasaidiwa na flash ya LED Flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Copper, Tempered Blue, Black
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint (Kwa Nyuma).
Bei ya Nokia X5 au Nokia 5.1 Plus
Kwa upande wa bei Nokia X5 ya GB 32 na RAM ya GB 3 itauzwa kwa Yuan ya China CNY 999 sawa na shilingi za Tanzania TSh 340,000 huku Nokia X5 ya GB 64 na RAM ya GB 4 yenyewe ikiwa inauzwa kwa Yuan ya China CNY 1,399 sawa na Shilingi za Tanzania TSh 475,000. Kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.
Na hiyo ndio simu mpya ya Nokia X5 ambayo imezinduliwa siku ya leo, Nokia imesema simu hizo zitanza kuuzwa kwa oda maalum kuanzia siku ya kesho tarehe 19 kupitia tovuti za Suning, JD, Lynx pamoja na kupitia tovuti ya Nokia.
Mko vizuri.hizo simu zipo hapa tz?
Nimejaribu pwa