in

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya za Huawei Nova 3

Zifahamu sifa na bei ya simu mpya za Huawei Nova 3 na Nova 3i

Sifa na Bei ya Huawei Nova 3 na Nova 3i

Kampuni ya Huawei mwaka huu 2018 bado inaendelea kuja na simu za kisasa na hapo jana kampuni ya Huawei imezindua simu mpya za Huawei Nova 3 na Huawei Nova 3i, simu zinazokuja na maboresho na sifa nzuri. Kwa mujibu wa tovuti ya Android Police, Simu hizi za Huawei Nova 3 ndio simu za kwanza kuwa na processor ya Kirin 970 chipset kwa Huawei Nova 3 na Kirin 710 kwa Huawei Nova 3i.

Japokuwa simu hizi za Huawei Nova 3 zinakuja na muonekano unao fanana na simu za Huawei P20 na Honor 10, lakini kwa upande wa sifa simu hizi ziko tofauti kabsa. Utofauti mkubwa wa Huawei Nova 3 na simu hizo uko kwenye processor za simu hizi, kwani simu hizi zinakuja na processor za Huawei za kirin 970 na kirin 710 processor ambazo zinakuja na uwezo mzuri wa teknolojia ya AI au Artificial intelligence.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sifa za Huawei Nova 3

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, 19.5:9 ratio (~409 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 na 4×1.8 GHz Cortex-A53), Hisilicon Kirin 970 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP12
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja ikiwa na GB 64 na nyingine ikiwa na GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa ukubwa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Ziko kamera mbili moja ikiwa na uwezo wa Megapixel 24 na nyingine ina Megapixel 2.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 16 yenye (f/1.8) na nyingine ikiwa na Megapixel 24 yenye B/W (f/1.8), gyro-EIS (1080p), na PDAF. Kamera zote mbili zinasaidiwa na flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3750 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 18W.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Blue, Purple na Gold.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint (Kwa Nyuma).

Tofauti na toleo la simu za Huawei Nova 2 ambazo zilikuja na matoleo mawili ya Huawei Nova 2 na Nova 2s, Sasa kampuni ya Huawei inakuja na toleo la Huawei Nova 3i toleo ambalo ndilo toleo la pili kwenye mfululizo wa simu za Huawei Nova 3.

Sifa za Huawei Nova 3i

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, 19.5:9 ratio (~409 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 na 4×1.8 GHz Cortex-A53), Hisilicon Kirin 710 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP12
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa ukubwa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Ziko kamera mbili moja ikiwa na uwezo wa Megapixel 24 na nyingine ina Megapixel 2.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 16 yenye (f/2.2, PDAF) na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye B(depth sensor). Kamera zote mbili zinasaidiwa na flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3340 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 10W.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Pearl White na Iris Purple.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint (Kwa Nyuma).

Simu zote mbili zinakuja na teknolojia ya AI kwenye kamera zake hivyo unaweza kupiga picha zenye rangi nzuri kulingana na mazingira uliyopo.

Bei ya Huawei Nova 3 na Bei ya Huawei Nova 3i

Kwa upande wa bei simu za simu hizi, Huawei Nova 3 inatarajiwa kuanzia dollar za marekani $445 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,015,000, huku kwa upande wa Huawei Nova 3i yenyewe ikianzia dollar za marekani $300 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 684,000. Kama kawaida kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Simu hizi zinatarajiwa kupatikana hivi karibuni huku Huawei Nova 3i ikianza kupatikana kuanzia siku ya leo tarehe 19 kupitia oda maalum na wateja watapata spika ya bure pale watakapo toa oda kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 27 mwezi huu. Unaweza kutoa oda yako hapa.

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya za Huawei Nova 3
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.