Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Watu 20 Wanaolipwa Pesa Nyingi Kuposti Tangazo Instagram

Hawa ndio watu wanaotumia akaunti zao za Instagram Vizuri..
Wanaolipwa Pesa nyingi instagram Wanaolipwa Pesa nyingi instagram

Mtandao wa instagram umebadilika sana toka ulipo anzishwa rasmi mwaka 2010, mwanzoni mtandao huu ulikuwa ni kwaajili ya matumizi binafsi na kila mtu alikuwa akitumia mtandao huo bila kupata faida yoyote. Miaka 8 baadae mtandao wa instagram umekuwa ni moja ya mitandao mihumu sana kwa sasa na watu wengi mbalimbali wamekuwa wakiendesha maisha yao kutokana na mtandao huo.

Sasa siku ya leo, Tanzania Tech tumekuandalia listi ya watu 20 wanaolipwa pesa nyingi zaidi kuposti tangazo kwenye akaunti zao za instagram. Kama unavyo hisi, asilimia 100 ya listi hii ni watu wanaojulikana sana na uhakika hata wewe umefuata (follow) akaunti ya Instagram ya mmoja ya watu hawa. Anyway bila kupoteza muda twende tukaangalie listi hii.

Advertisement

20. Huda Kattan

Analipwa Euro £25,100 sawa na Tsh Milioni 75 Kwa Posti Moja. Huda Kattan ni mjasiri ya mali, blogger pamoja na mkurugenzi mtendaji wa kampuni yake ya vipodozi ya Huda Beauty.

19. Floyd Mayweather

Analipwa Euro £81,400 sawa na Tsh Milioni 244 kwa Posti Moja. Floyd Joy Mayweather Jr, ni bondia mstaafu na pia kwa sasa ni promoter wa maswala hayo ya ubondia.

18. Stephen Curry

Analipwa Euro £83,700 sawa na Tsh Milioni 251 kwa Posti Moja. Stephen Curry ni mchezaji wa mpira wa kikapu nchini marekani kupitia timu ya Golden State Warriors. Stephen Curry anajulikana sana kwa uwezo wa wake mkubwa kuingiza mipira mingi kapuni kwenye NBA, a.k.a greatest shooter in NBA history.

17. Virat Kohli

Analipwa Euro £91,280 sawa na Tsh Milioni 273 kwa Posti Moja. Virat Kohli ni mchezaji wa mchezo wa cricketer wa nchini India.

16. Conor Mcgregor

Analipwa Euro £95,100 sawa na Tsh Milioni 285 kwa Posti Moja. Conor Anthony McGregor ni mtaalamu wa ngumi pamoja na mbinu za kupigana (mixed martial artist) kutokea nchini Ireland.

15. Luis Suarez 

Analipwa Euro £117,900 sawa na Tsh Milioni 353 kwa Posti Moja. Luis Alberto Suárez Díaz ni mchezaji wa soka au mpira wa miguu wa Uruguay ambaye anacheza kama mshambuliaji kwenye klabu ya Hispania Barcelona na timu ya taifa ya Uruguay.

14. Zlatan Ibrahimovic

Analipwa Euro £133,000 sawa na Tsh Milioni 398 kwa Posti Moja. Zlatan Ibrahimović ni mchezaji wa soka wa Kiswidi ambaye anacheza kama mchezaji wa mbele kwenye klabu ya LA Galaxy.

13. Gareth Bale

Analipwa Euro £140,700 sawa na Tsh Milioni 421 kwa Posti Moja. Gareth Frank Bale ni mchezaji wa kitaalamu wa Welsh ambaye anacheza kama winger kwenye klabu ya Hispania Real Madrid na timu ya taifa ya Wales.

12. David Beckham

Analipwa Euro £228,200 sawa na Tsh Milioni 682 kwa Posti Moja. Daudi Robert Joseph Beckham OBE ni mchezaji wa soka mstaafu wa Kiingereza. Alicheza Manchester United, Preston North End, Real Madrid, Milan, LA Galaxy, Paris Saint-Germain na England.

11. Khloe Kardashian

Analipwa Euro £365,000 sawa na Tsh Bilioni 1 kwa Posti Moja. Khloé Alexandra Kardashian ni mwana televisheni wa Marekani,sociallite, mfanyabiashara, na mjasiriamali. Tangu mwaka 2007, amekuwa nyota yeye na familia yake katika tamthilia halisi ya televisheni ya Keeping Up with the Kardashians.

Top 10 Watu Wanaolipwa Pesa Nyingi Kuposti Tangazo Instagram

Baada ya kuangalia watu kumi wa mwisho kwenye watu hawa 20 sasa twende tukangalie Top 10 ya watu wanaolipwa Pesa nyingi zaidi kwa kupoti tangazo kupitia akaunti zao za mtandao wa Instagram. Bila kupoteza muda Lets Goo.

10. Kendall Jenner

Analipwa Euro £380,200 sawa na Tsh Bilioni 1.1 kwa Posti Moja. Kendall Nicole Jenner ni mrembo (model) wa marekani pamoja na mwana televisheni. Alianza Kuonekana kwa awali katika televisheni ya E! kupitia tamthilia ya ukweli ya Keeping Up with the Kardashians.

9. Lionel Messi

Analipwa Euro £380,200 sawa na Tsh Bilioni 1.1 kwa Post Moja. Lionel Andrés Messi Cuccittini ni mchezaji wa soka wa Argentina ambaye anacheza kama mchezaji wa mbele wa klabu ya Hispania Barcelona na timu ya taifa ya Argentina.

8. Neymar Jr

Analipwa Euro £456,200 sawa na Tsh Bilioni 1.3 kwa Post Moja. Neymar da Silva Santos Junior ni mchezaji wa soka wa Brazil ambaye anacheza kama mchezaji wa mbele wa klabu ya Kifaransa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Brazil.

7. Justin Bieber

Analipwa Euro £479,000 sawa na Bilioni 1.4 kwa Posti Moja. Justin Drew Bieber ni mwimbaji wa Canada, mwigizaji na mtunzi. Alikuwa maarufu zaidi baada ya meneja wa vipaji kumgundua kupitia video zake za YouTube mwaka 2008.

6. Dwayne Johnson

Analipwa Euro £494,300 sawa na Bilioni 1.47 kwa Posti Moja. Dwayne Douglas Johnson, ambae pia anajulikana kwa jina lake la The Rock, ni mwigizaji wa Marekani, mtayarishaji, na wrestler mstaafu.

5. Beyonce

Analipwa Euro £532,000 sawa na Bilioni 1.5 kwa Posti Moja. Beyoncé Giselle Knowles-Carter ni mwimbaji wa Marekani, mwandishi, dancer, mwigizaji, na mfanyabiashara.

4. Kim Kardashian

Analipwa Euro £547,000 sawa na Bilioni 1.6 kwa Posti Moja. Kimberly Kardashian West ni mwana televisheni wa Marekani, mrembo, sociallite, mfanyabiashara, na mjasiriamali.

3. Cristiano Ronaldo

Analipwa Euro £570,000 sawa na Bilioni 1.7 kwa Posti Moja. Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro GOIH ComM ni mchezaji wa soka wa Kireno ambaye anacheza kama mchezaji wa mbele wa klabu ya Italia Juventus na timu ya Taifa ya Ureno.

2. Selena Gomez

Analipwa Euro £608,000 sawa na Bilioni 1.8 kwa Posti Moja. Selena Marie Gomez ni mwimbaji wa Marekani, mwigizaji, na mtayarishaji. Alikuwa maarufu zaidi baada ya kuonekana kwenye mfululizo wa vipindi vya televisheni vya watoto Barney & Friends.

1. Kylie Jenner

Analipwa Euro £760,000 sawa na Bilioni 2.2 kwa Posti Moja. Kylie Kristen Jenner mwana televisheni wa Marekani, mrembo, sociallite, mfanyabiashara, na mjasiriamali. Huyu ndio anaye ongoza kwa sasa kwa kulipa pesa nyingi zaidi kuposti posti moja ya Tangazo la biashara kupitia mtandao wa Instagram.

Na hiyo ndio listi ya watu wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi kwa kuposti tangazo kwenye akaunti zao za instagram kwa mujibu wa tovuti ya The Sun, Kwa hapa Tanzania bado hakuna utafiti kama huu lakini pengine lazima mwana muziki Diamond Platnumz, atakuwa kwenye nafasi ya kwanza au kwenye kumi bora. That’s it Guys endelea kutembelea Tanzania Tech kwa habari zaidi za Teknolojia.

4 comments
  1. Mko moto hatari, hivi inakuaje au ni system gani wanatumia mpaka wanalipwa kias hicho chote?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use