Muonekano wa Galaxy Tab S4 Wavuja Kabla ya Kuzinduliwa

Huu ndio Muonekano halisi wa tablet mpya ya Samsung Galaxy Tab S4
Galaxy Tab S4 Galaxy Tab S4

Sio muda mrefu sana umepita kutoka kampuni ya Samsung ilipo zindua toleo la mwisho la Galaxy Tab S3, toleo hili lilizinduliwa rasmi mwezi Aprili mwaka uliopita 2017. Japokua mpaka sasa bado toleo jipya la Galaxy Tab S4 halijatoka rasmi, lakini kumekuwa na tetesi mbalimbali kuhusu tablet hiyo ambayo sasa picha yenye muonekano wake imevuja rasmi.

Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali kupitia tovuti mbalimbali, muonekano huu ndio muonekano halisi wa tablet hiyo inayotegemewa kuzinduliwa siku za karibuni. Kwa muonekano wa picha hiyo tablet hiyo inakuja na maboresho mengi huku ikiwa na kioo cha kikubwa kisicho na kingo kubwa (bezels).

Kwa muonekano wa picha hiyo kitu cha kwanza unachoweza kuona ni kuwa Galaxy Tab S4 haina kibonyezo cha katikati, pia kwa kuangalia kioo cha tablet hiyo utaona kioo chake ni kikubwa zaidi huku kikiwa na kingo ndogo zaidi ukilinganisha na tablet ya Galaxy Tab S3.

Advertisement

Hata hivyo kukosekana kwa kitufe cha katikati kunaleta swali je sehemu ya ulinzi ya Fingerprint itakuwa wapi..? Je Samsung wataweka sehemu hiyo chini ya kioo au itakuwa kwa pembeni au Galaxy Tab S4 itakuja bila sehemu ya Fingerprint .?, kwa sasa hakuna aliye na majibu ya maswali haya itabidi tusubiri ili kuweza kujua zaidi.

Tukiachana na hayo na kubakia upande wa mbele wa tablet hii, tunaona sehemu ya kamera ya mbele pamoja na sensor ambayo inasemekana kuwa inawezekana ni kwaajili ya Iris scanner ambayo inawezekana ndio sababu ya kukosekana kwa sehemu ya fingerprint. Iris scanner hufanya kazi ya kuwezesha mtu kufungua simu yake kwa kutambua uso.

Kwa upande wa sifa, Tablet hii ya Galaxy Tab S4 inasemekana inakuja na processor ya Snapdragon 835 chipset na inasemekana itakuja na kioo cha Inch 10.5 chenye teknolojia ya WQXGA pamoja na resolution ya 2560 x 1600 pixels yenye aspect ratio ya 16:10. Kwa upande wa ukubwa wa ndani Galaxy Tab S4 inasemekana kuja na ukubwa wa GB 64GB huku ikisaidia wa RAM ya GB 4.

Kamera za Galaxy Tab S4 zinasemekana kuwa na Megapixel 12 kwa kamera ya nyuma na Megapixel 7 kwa kamera ya mbele. Battery ya tablet hii inasemekana kuwa na uwezo wa 7,300mAh, mfumo wa Android 8.1 (Oreo) ndio unasemekana kuendesha tablet hiyo ambayo inasemekana kuzinduliwa rasmi tarehe 24 mwezi wa nane mwaka huu 2018.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use