Hapo siku ya jana kampuni ya Apple imetangaza kufanya maboresho ya laptop zake za Macbook Pro, maboresho yaliofanyika ni pamoja na kuboresho wa vioo vya laptop hizo, aina mpya za vichapishio (keyboard) pamoja na maboresho ya mbalimbali ya uwezo.
Hata hivyo laptop za Macbook ambazo zimefanyiwa maboresho haya ni zile laptop ambazo ni za bei ghali, nikisema bei ghali hapa nazungumizia Macbook Pro ya Inch 13 na ile ya inch 15 zenye Touch Bars. Kwa sasa bado hakuna taarifa za maborasho ya matoleo ya laptop za kawaida za Macbook Pro ambazo hazina Touch Bar.
Sasa tukija kwenye mabadiliko yenyewe, Apple imefanya mabadiliko ya Macbook Pro ya Inch 15 yenye Touch Bar kwa kuongeza processor za core i7 na Core i9 huku kompyuta hizo kwa sasa zikiwa na uwezo wa kuongezewa RAM ya DDR4 hadi kufikia GB 32. Pia ukubwa wa ndani wa laptop hii umeongezwa hadi kufikia Terabyte 4. Tukirudi tena kwenye Processor ya laptop hii, Macbook Pro ya Inch 15 inakuja na uwezo wa 2.9GHz huku ikiwa na uwezo wa Turbo Boost yenye uwezo wa 4.8GHz.
Kwa upande wa Graphic, laptop hii ya Macbook Pro ya Inch 15 imefanyiwa maboresho ya GPU na sasa itakuwa na Graphics ya Radeon Pros yenye uwezo wa hadi GB 4. Bei Macbook Pro yenye maboresho haya imesimamia kucha kuanzia dollar za marekani $6,699 ambayo ni sawa na Tsh Milioni 15,254,000 za Tanzania.
Kwa upande wa laptop ya Inch 13 yenye Touch Bar, yenyewe imefanyiwa maboresho machache ya processor za core i5 na Core i7 zenye speed kuanzia 2.7GHz hadi 4.5GHz Turbo Boost. Maboresho mengine ni pamoja na ukubwa wa hard disk umeongezwa hadi TB 2. Bei ya Laptop hii yenyewe iko palepale kuanzia dollar za marekani $1,799 sawa na Tsh 4,095,000. Kwa ufupi hapo chini ni mabadiliko makubwa yalio fanyika kwenye laptop hizo.
Maboresho ya MacBook Pro Inch 15
- Processor – Processor 6-core Intel Core i7 au Core i9 processors yenye speed ya 2.9GHz yenye Turbo Boost hadi 4.8GHz
- RAM – Hadi GB 32 DDR4 memory
- Graphics – Radeon Pro discrete graphics yenye GB 4 za video memory
- Ukubwa wa Ndani – 4TB ya SSD storage
Maboresho ya MacBook Pro Inch 13
- Processor – Quad-core Intel Core i5 au i7 processors yenye speed ya 2.7GHz ikiwa na Turbo Boost hadi 4.5GHz
- Graphics – Intel Iris Plus 655 integrated graphics with 128MB of eDRAM
- Ukubwa wa Hard Disk – Hadi TB2 SSD storage
Mbali na maboresho haya makubwa, Apple pia imeleta maboresho ya vioo vya laptop hizi kwa kuongeza teknolojia ya True Tone display ambayo hii inasaidia kioo cha laptop yako kujiweka rangi sahihi kulingana na hali ya chumba au mahali unapo itumia laptop hiyo. Mbali na hayo pia laptop hizi ndio zitakuwa laptop za kwanza kutumia programu ya SIRI kwa kusema maneno ya Hey Siri tofauti na laptop za sasa ambazo ni lazima kubofya vitufe maalum.
Na hayo ndio maboresho yalifanyika kwenye laptop hizo za Macbook Pro, bado hakuna taarifa lini laptop hizo zitapatikana rasmi lakini kwa mujibu wa ripoti mbalimbali huwenda laptop hizi zikapatikana kuanzia mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao… Hivyo Basi Andaa Pochi..
Nice asante kwa Habari, keep up
Bei gani hizo zitakuwa zinauzwa?