Instagram umekuwa ni mtandao wa muhimu sana kwa biashara mbalimbali, iwe ni kampuni au hata watu binafsi instagram kwa sasa ni moja ya mtandao wa kijamii ambao ni muhimu sana kuwa na akaunti na hii inatokana na kuwepo kwa watumiaji wengi wa mtandao huo.
Pamoja na kuwepo kwa umuhimu wa kuwa na akaunti kwenye mtandao huo lakini bado akaunti yako iwe ya kibiashara au akaunti binafsi inakuwa haina nguvu mpaka hapo itakapo pata tiki ya blue au kuwa (Verified). Hata hivyo kupata tiki hiyo ya blue au kuwa (Verified) imekuwa ni kazi ngumu sana na hii inatokana na ugumu wa kufanya uhakiki huo wanaoupata instagram.
Sasa ili kuwezesha uhakiki wa akaunti hizo kuwa mrahisi, Instagram inakuja na sehemu mpya na rahisi kutumia ya kuwezesha wamiliki wa akaunti hizo kuomba uhakiki moja kwa moja kupitia akaunti zao za mtandao wa instagram.
Sehemu hiyo kwa sasa iko kwenye hatua za majaribio na kupitia sehemu hiyo mtumiaji anatakiwa kutuma data zake za muhimu kama vile jina kamili pamoja na kitambulisho cha utaifa au kitambulisho chochote kilichotolewa na serikali na ambacho kinaonyesha picha ya sura yako pamoja na tarehe ya kuzaliwa.
Kwa sasa bado hakuna utaratibu uliotajwa ambao utatumika kuhakiki akaunti za kibiashara ili kupata tiki ya blue, lakini inasemekana instagram itatumia kitambulisho hicho hicho au leseni ya biashara kuweza kuhakiki akaunti za aina hiyo.
Hata hivyo bado yapo mambo ambayo Instagram wanaangalia ili kuweza kutoa uhakiki huo mara baada ya wewe kuomba kwa kutumia njia hii. Kama ungependa kujua mambo hayo ili kupata tiki ya blue endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha mambo yote na njia ambazo unatakiwa kufuata ili kuhakikisha unapata tiki hiyo ya blue kwenye akaunti yako.
Kwa sasa sehemu hii inapatikana kwa watumiaji wa mtandao wa Instagram wa nchini Australia huku sehemu hiyo ikiwa inapatikana kwanza kupitia programu ya instagram ya mfumo wa iOS.
Nawapenda bure
Karibu
Naomba nielekezwe jins ya kupata tiki ya blue