Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Instagram najua utakuwa umeona sehemu mpya kwenye mtandao wa Instagram, sehemu hii itaweza kuonyesha kama mtu yupo online kwenye mtandao huo wa instagram.
Sehemu hiyo ambayo sasa inapatikana kwenye mtandao huo, itaonyesha kidoti cha kijani pembeni ya jina la mtu kupitia sehemu ya DM ambapo kidoti hicho kitakuwa na maana mtu yuko hewani (Online) kwa muda huo kwenye mtandao wa Instagram. Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, kidoti hicho cha kijani kitakuwa kinaonekana kwenye baadhi ya sehemu mbalimbali kama vile sehemu ya DM pamoja na wakati wa kushare picha na mfuasi (Follower) wako au mtu unae mfuata (Follow).
Instagram imekuwa ikibadilisha matumizi ya sehemu ya DM mara kwa mara, kwani siku za karibuni Instagram ilitambulisha App ya Direct kwaajili ya kuchati kupitia mtandao huo ikifuatiwa na sehemu ya kujua mtu alikuwa hewani kwa muda gani uliopita. Pengine hizi ni hatua za kubadilisha sehemu hiyo ya DM kuwa sehemu ya kuchati kama vile app za WhatsApp pamoja na Facebook Messenger.
Kwa sasa sehemu hii ya kidoti cha kijani inapatikana tayari kwenye App za mifumo yote ya Android pamoja na iOS. Kwa mujibu wa ripoti sehemu hii itatokea kwa watu uliowafuata (Follow) au walio kufuata (Followers) ikiwa pamoja na watu ambao tayari ulisha chati nao kupitia sehemu ya DM.