Instagram imekuwa na maboresho mengi sana hivi sasa, baada ya kusikia ujio wa IGTV, programu mpya ya Instagram Lite, na kuongezwa kwa sehemu mpya kwenye app ya instagram, sasa instagram imeongeza sehemu nyingine ambayo itakuwezesha kuuliza maswali kupitia sehemu ya Stories.
Tofauti na sehemu ya Sticker poll inavyofanya kazi, sehemu hiyo mpya ya kuuliza maswali yenye itakupa uwezo wa kuandika jibu kabisa tofauti na sehemu ya Sticker Poll ambayo ni lazima ujibu swali kwa kupandisha na kushusha emoji husika.
Kama unavyo ona hapo juu, picha hiyo inaonyesha sehemu hiyo itakuwa inaruhusu watumiaji kuweza kujibu maswali kwa kuandika majibu yao moja kwa moja kupitia sehemu ya Stories. Bado hakuna taarifa kama kutakuwa na kiwango maalum cha idadi ya maneno yatakayo kuwa yanaweza kuandikwa kupitia sehemu hiyo, na pia bado hakuna taarifa kuhusu lini sehemu hiyo itakuja kwenye programu za Instagram.
Kwa mujibu wa tovuti ya Android Police kwa sasa ni watu wachache wenye uwezo wa kuona sehemu hiyo, hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuhabarisha zaidi na hakikisha unasasisha toleo jipya la app ya instagram pindi inapo toka kupitia masoko ya Play Store pamoja na App Store.