Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

WhatsApp ya Biashara Kuja na Uwezo wa Kuuza Bidhaa

Sasa utaweza kuonyesha bidhaa zako ndani ya programu hiyo
WhatsApp ya biashara kuuza bidhaa WhatsApp ya biashara kuuza bidhaa

WhatsApp ya Biashara ni moja kati ya programu muhimu sana kwa wale wanaopenda kutenganisha maisha yao binafsi na kazi. Tofauti na WhatsApp ya kawaida, programu hii inamuwezesha mtumiaji kutengeneza profile maalum yenye namba za simu, tovuti, anwani mahali biashara ilipo pamoja na ramani yenye kuonyesha eneo biashara inapo patikana.

Hata hivyo programu hii imeendelea kuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara mbalimbali na hivi karibuni programu hiyo inategemewa kuwa msaada zaidi hasa kwa wale wanaofanya biashara mtandaoni.

Advertisement

Kwa mujibu wa habari kutoka tovuti ya WABetaInfo, hivi karibuni watumiaji wa WhatsApp ya biashara wataweza kuonyesha na kuuza bidhaa zao moja kwa moja kupitia programu hiyo, watumiaji wateweza kuweka data muhimu za bidhaa zao wanazouza mtandaoni ikiwa ni pamoja na jina la bidhaa, maelezo ya bidhaa, namba ya utambulisho wa bidhaa (SKU), bila kusahau picha za bidhaa pamoja na link kwenda kwenye tovuti inayo uza bidhaa hiyo.

Hata hivyo bado haijajulikana moja kwa moja kama sehemu hii itaruhusu mtumiaji kuweka bei ya bidhaa ili kuuza bidhaa ndani ya programu hiyo au mtumiaji analazimika kununua bidhaa kupitia link ya tovuti husika. Hata hivyo inawezekana mtumiaji kuuza bidhaa ndani ya programu hiyo kwani hivi karibuni WhatsApp ilizindua njia ya malipo nchini india, ambapo mtumiaji wa programu hiyo anaweza kutuma pesa kwenye huduma au kwa mtu binafsi moja kwa moja kwa kutumia programu ya WhatsApp.

Mbali na hayo, Habari nyingie pia zinasema programu ya WhatsApp ya Biashara inatarajia kuongezewa njia ya kutenganisha meseji kwa vipengele ili kurahisisha mtumiaji wa programu hiyo kuweza kujua tofauti ya meseji kama vile, meseji za malalamiko, meseji za kuomba msaada, pamoja na meseji za maoni. Hata hivyo bado haijajulikana lini toleo lenye maboresho haya litatoka rasmi lakini inasemekana ni kuanzia mwezi huu. Kwa sasa kama unataka kuuza bidhaa kupitia WhatsApp unaweza kusoma hapa.

Kwa sasa WhatsApp ya biashara inapatikana kwa watumiaji wa Android pekee, huku watumiaji wa mfumo wa iOS wakitegemea kupata programu hiyo kwenye siku za karibuni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use