Uchunguzi Waanza kwa Wanaotuma Meseji za Kitapeli

Wanaotuma meseji za kitapeli Tanzania sasa kubainika
meseji za kitapeli meseji za kitapeli

Ripoti kutoka kwenye tovuti ya Mwananchi zinasema kuwa, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandaoni, (Cybercrime investigation unit) kinafanya uchunguzi kuwabaini wanaotuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi kwa nia ya kuwatapeli wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Barnabas Mwakalukwa, leo Juni 6, imesema yeyote aliyetapeliwa anatakiwa kutoa taarifa kwani jumbe hizo zina lengo la kuwatapeli na kuwaibia fedha wananchi.

“Tunawataka wananchi kuacha kutumia simu na mitandao ya kijamii vibaya na badala yake itumike kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo,” imesema taarifa hiyo.

Advertisement

Taarifa hiyo imesema, baadhi ya jumbe hizo ni zile zinazosema. ‘Ile hela tuma kwa namba hii’ au ‘usipige kwa sasa, spika imeharibika, tuma ujumbe,’ au ‘Mjukuu wangu ile ndagu niliyokutumia imefanya kazi na sasa unapata wateja wengi… sasa njoo uchukue ndagu nyingine ya mvuto.’

Taarifa kutoka tovuti ya Mwananchi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use