Tetesi : Infinix Kuja na Simu Mpya ya Infinix Note 5 Mwezi Huu

Baada ya Infinix Hot 6 sasa jiande na Infinix Note 5
Infinix Note 5 Infinix Note 5

Wakati ikiwa bado simu za Infinix Hot 6 ni mpya mbele ya macho ya watu wengi, tayari tetesi mpya zimesha ibuka kuhusu ujio wa simu mpya ya Infinix Note 5. Kwa mujibu wa tetesi simu hiyo inatarajiwa kuja mwezi huu na inatarajiwa kuja na muonekano mzuri zaidi.

Kampuni ya Infinix ni moja kati ya kampuni inayo tengeneza simu za bei nafuu, lakini pia kwa mwaka huu kampuni hiyo imeonekana kubadilika kwa haraka sana na kuja na simu zenye sifa bora na ambazo ni za bei nafuu.

Tumesha zoea kusikia, kampuni hizi nyingi hutumia processor za Mediatek chipset ambazo ni processor za kawaida ukilinganisha na processor za Snapdragon chipset ambazo kampuni ya infinix imeanza kutumia kwenye simu ya Infinix Hot 6. Sasa kwa mujibu wa tetesi hizo bado hakuna taarifa kama kampuni hiyo itatumia processor hizo kwenye simu hiyo ya Infinix Note 5, lakini ni wazi simu hiyo itakuwa na muundo mzuri ukizingatia jina la simu hiyo litakuwa ni Infinix Note 5 Stylus.

Advertisement

Hata hivyo tetesi hizo zinasema simu hiyo inategemewa kuja na battery kubwa ya 4300mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji zaidi ya siku moja kulingana na matumizi yako. Vilevile simu hii inasemekana kuja na kamera ya mbele ya Megapixel 8 pamoja na kamera ya megapixel 13 kwa nyuma. Simu hii inatarajiwa kuja na mfumo wa AndroidONE 8.1.

Mbali na hayo simu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya jumapili ya tarehe 24 mwezi huu wa sita huko nchini Dubai, endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi.

3 comments
  1. nafurahi kwa ujio huo wa note5,tatizo langu ni kwenye hii infinix note4 pro ninayoitumia haikamati network inakuandikia cellular data not available sasa tatizo ni nini! naomba msaada wataalamu wa Tanzania tech,asante.

    1. Habari Leonard, Swali ulilo uliza hapa ni la kitaalamu zaidi, Tafadhali nenda kwa wakala wa simu za infinix au wasiliana nao kwa namna ya simu au kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use