Kampuni ya Tecno imekuwa ni moja kati ya kampuni yenye kuuza simu za bei nafuu zaidi hapa Afrika, kwa sababu hii kampuni ya Tecno imezidi kukuwa kila siku na hivi karibu hayo yamebainishwa baada ya ripoti kutoka Brand Africa ambao wametoa ripoti inayoonyesha bidhaa za Afrika zinazopendekezwa zaidi kwa mwaka huu 2018.
Katika ripoti hiyo ambayo imehusisha kampuni mbalimbali, kampuni ya Tecno imeonekana kushika namba 7 kutoka namba 14 kwenye ripoti ya mwaka jana ya bidhaa zenye kukubalika zaidi Afrika huku ikipita kampuni mbalimbali kama Google, Huawei pamoja na Nokia ambazo zimeshuka zaidi.
Hata hivyo chini ya kipengele cha eletroniki na kompyuta (electronics and computers), kampuni ya Tecno imeshika namba 3 tatu huku ikiwa chini ya kampuni za Samsung pamoja na Apple.
Mbali na hayo kwenye ripoti hiyo Google imeshika namba moja, kwenye kipengele cha Media, huku ikifuatiwa na Dstv kwenye nafasi ya pili na kwenye nafasi ya tatu ikiwa kampuni ya Facebook.
Kwa hapa Tanzania iko kampuni moja tu ya Azam ambayo imeshika namba 3 kwenye kipengele cha Chakula, huku kwenye list ya bidhaa zinazokubalika zaidi Afrika (2018) ikiwa imeshika namba 51. Kwenye kipengele cha Mawasiliano hakuna kampuni yoyote ya Tanzania huku kampuni za MTN ya South Afrika na Airtel ya India zikiwa zinaongoza kukubalika kwa hapa Afrika.