Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sifa na Bei ya Simu Mpya za Tecno Pouvoir 2 na Pouvoir 2 Pro

Simu hizi zinauwezo wa kudumu na chaji hadi masaa 96
Sifa na Bei ya TECNO Pouvoir 2 Sifa na Bei ya TECNO Pouvoir 2

Wakati tukiwa bado tunasubiri kampuni ya Tecno kuzindua simu ya Spark 2, Hivi karibuni Tecno imezindua simu mpya za Tecno Pouvoir 2 na Tecno Pouvoir 2 Pro, simu hizi zinakuja kama sehemu ya maboresho ya simu ya Pouvoir 1, simu ambayo ilizinduliwa na Tecno kimya kimya hapo mwezi wa nne mwaka huu 2018.

Simu hizi za Pouvoir 2 na Pouvoir 2 Pro, zinakuja na maboresho mengi ikiwemo, RAM ya GB 2 kwa Pouvoir 2 na RAM ya GB 3 kwa Pouvoir 2 Pro, simu hizi pia zinakuja na ukubwa wa ndani wa GB 16, kioo cha inch 6.0 chenye teknolojia ya HD, huku simu zote mbili zikiendeshwa na mfumo wa undeshaji wa Android Oreo 8.1.

Advertisement

Kwa upande wa kamera simu hizi zinakuja na Kamera ya Megapixel 8 kwa mbele na Megapixel 13 kwa nyuma kwa simu ya Tecno Pouvoir 2, huku Tecno Pouvoir 2 Pro yenyewe ikiwa na kamera ya mbele ya Megapixel 13 kwa mbele pamoja na Megapixel 13 kwa nyuma. Mbali na hayo simu hii inakuja na battery kubwa ya mAh 5000 yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa masaa 96, Sifa nyingine za simu hizi ni kama zifuatavyo.

Sifa za Tecno Pouvoir 2

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya HD+ IPS LCD capacitive touchscreen display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1720 x 1440 pixels (~269 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.3GHz, MediaTek MT6737 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-T720 MP2
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na Memory Card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 8, yenye LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 5000 mAh
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za City Blue, Midnight Black, Champagne Gold
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Simu ya Tecno Pouvoir 2  na Tecno Pouvoir 2 Pro hazi tofautiani hata kidogo kwa muonekano, bali tofauti kubwa iliyopo kwenye simu hizi ni kwenye sifa za ndani ambapo RAM, Processor na kamera za Pouvoir 2 Pro ni kubwa zaidi.

Sifa za Tecno Pouvoir 2 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya HD+ IPS LCD capacitive touchscreen display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1720 x 1440 pixels (~269 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.5GHz, MediaTek MT6750 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-T860 MP2
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na Memory Card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 13 yenye LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 5000 mAh
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za City Blue, Midnight Black, Champagne Gold
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Tecno Pouvoir 2 na Pouvoir 2 Pro

Kwa upande wa bei za simu hizi, Pouvoir 2 itakuja ikiwa inauzwa kwa makadirio ya Shilingi za Kitanzania Tsh 310,000 wakati Tecno Pouvoir 2 Pro yenyewe itauzwa kwa makadirio ya Tsh 350,000. Kwa sasa simu hizi zinapatikana kupitia soko la Jumia la nchini Nigeria, huenda zikaja na hapa Tanzania Siku za karibuni.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use