Kampuni ya simu ya Oppo ambayo pia ni sehemu ya kampuni ya One Plus, hivi karibuni imezindua simu yake mpya ya kisasa inayoitwa Oppo Find X, Simu hii inakuja na aina mpya ya kamera pamoja na kioo kikubwa kisichokua na ukingo. Oppo find X inakuja na kioo cha inch 6.4 chenye teknolojia ya Super Amoled chenye uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16.
Mbali na hayo uzuri wa simu hii haubaki kwenye kioo pekee bali pia kwenye mfumo wake wa kamera. Oppo find X inakuja na mfumo wa kisasa wa kamera ambapo kamera zake zinajificha kwa nyuma ya simu hii na pele utakapo taka kuchukua picha au video ndipo kamera hizo hufunguka kutoka kwenye kava maalum nyuma ya simu hiyo.
Mbali na hayo simu hii inakuja na muonekano kama simu ya Samsung Galaxy S9 Plus, ambayo inafanana na simu hii kwa sababu ya muonekano wake wa kioo chenye kujikunja kwa pembeni. Sifa nyingine za Oppo Find X ni kama zifuatazo.
Sifa za Oppo Find X
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, 19.5:9 ratio (~403 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver), Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Adreno 630
- Ukubwa wa Ndani – Ziko tatu moja ina GB 64, nyingine GB 128 na nyingine ina GB 256 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
- Ukubwa wa RAM – Ziko mbili moja ikiwa na GB 8 na nyingine ikiwa na GB 6
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye (f/2.0).
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/2.0) na nyingine ikiwa na Megapixel 20 yenye (f/2.0), huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, dual-LED dual-tone flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3730 mAh battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging) (VOOC Flash Charge 5V/4A).
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, 3.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Bordeaux Red, Glacier Blue.
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa kutambua uso (Face ID) Haina Fingerprint.
Bei ya Oppo Find X
Oppo Find X inakuja kwa matoleo matatu tofauti yenye ukubwa wa ndani tofauti hivyo ni wazi bei itakuwa inatofautiana kwa kila simu kulingana na ukubwa wake wa ndani. Kwa sasa bei ya simu hii bado haija tangazwa rasmi ila endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha pindi tutakapo pata bei halisi ya simu hii.
Bado bei ya oppo find x haijatangazwa??nilikuwa nataka kujua bei yake
Tayari