Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sifa na Bei ya Simu Mpya za Infinix Note 5 na Note 5 Pro

Kampuni ya Infinix imerudi tena na simu mpya ya Infinix Note 5
Sifa na Bei ya Infinix Note 4 na Note 5 Pro Sifa na Bei ya Infinix Note 4 na Note 5 Pro

Baada ya tetesi za ujio wa simu mpya za Infinix Note 5, Hapo siku ya jana huko nchini Dubai kampuni ya Infinix imezindua rasmi simu hizo za Infinix Note 5 pamoja na Infinix Note 5 Pro, simu hizi zinakuja na muundo mzuri zaidi kuliko simu za mwaka jana za Infinix Note 4 pamoja na kamera zenye teknolojia ya (AI) au Artificial Intelligence, pamoja na mfumo wa uendeshaji wa Android One.

Simu hizo pia zinaingia kwenye historia ya kampuni hiyo kwa kuwa simu za kwanza kabisa kutoka kampuni ya Infinix kuwa na teknolojia ya AI kwenye kamera zake. Teknolojia hiyo inawezesha kamera hizo kutambua mazingira ya picha ili kuweza kuchukua picha bora zenye rangi nzuri zaidi.

Advertisement

Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji wa Infinix Note 5 na Note 5 Pro, simu hizi zinakuja na mfumo wa Android One Oreo 8.1, mfumo ambao unatoka moja kwa moja kutoka Google hivyo watumiaji wa Infinix Note 5 au Infinix Note 5 Pro wataona kama vile wanatumia simu za Google Pixel. Kingine kizuri kuhusu mfumo wa Android One ni pamoja na kuwepo kwa teknolojia ya AI moja kwa moja kwenye mfumo huo, na mfumo huo mara nyingi unakuja na programu za muhimu kutoka Google.

Sifa za Infinix Note 5

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS FHD LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 X 2160 pixels, 18:9 ratio (~407 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android One 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz, MediaTek Helio P23 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali G71 MP2
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 12 yenye LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 16 yenye dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4500 mAh battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, 3.0, microUSB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Milan Black, Berlin Gray na Ice Blue colors..
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint. (Kwa Nyuma)

Tofauti ya Infinix Note 5 na Infinix Note 5 Pro ni ndogo lakini inayoonekana kwani Infinix Note 5 pro inakuja na kalamu maalum ambayo unaweza kutumia kama ilivyo Galaxy Note 9 au Samsung Galaxy Note 8, Vilevile Note 5 Pro inakuja na RAM kubwa pamoja na ukubwa wa ndani mkubwa zaidi. Hapo chini ni sifa za Infinix Note 5 Pro.

Sifa za Infinix Note 5 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS FHD LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 X 2160 pixels, 18:9 ratio (~407 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android One 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz, MediaTek Helio P23 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali G71 MP2
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 12 yenye LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 16 yenye dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4500 mAh battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, 3.0, microUSB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Milan Black, Berlin Gray na Ice Blue colors..
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack, pamoja na Kalamu.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint. (Kwa Nyuma)

Bei ya Infinix Note 5 na Infinix Note 5 Pro

Kwa upande wa bei ya simu hizi, simu ya Infinix Note 5 inakuja ikiwa inauzwa kwa shilingi za kenya KSh 17,939 sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 410,000. Kwa upande wa simu mpya ya Infinix Note 5 Pro simu hii bado haija tangazwa bei yake ila inasemekana bei yake bei yake inategemewa kuanzia Tsh 450,000 hadi Tsh 500,000.

10 comments
  1. Mbona me najaribu kufungua data kwenye simu yangu ya infinix Note 5 haifunguki data niliyonunua juzi? naombeni usadizi kutoka kwenu

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use