in

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy J3 (2018) na J7 (2018)

Mabadiliko ya simu hizi ni machache sana..

Sifa na bei ya galaxy J3 (2018)

Kampuni ya Samsung imerudi tena mwezi huu na kipindi hichi Samsung inakuja na matoleo mapya ya simu za Samsung Galaxy J3 (2018) na Samsung Galaxy J7 (2018). Simu hizi ni maboresho ya simu za Galaxy J3 (2017) na J7 (2017) ambazo zilizinduliwa mwaka jana mwezi kama huu.

Mwaka huu Galaxy J7 (2018) inakuja na sifa zinazo fanana na simu ya J7 ya mwaka jana tofauti iliyopo ni kwenye upande wa kamera kwani simu hii inakuja na kamera ya Megapixel 13 kwa mbele pamoja na nyuma pia inakuja na kamera ya Megapixel 13. Kwa upande wa sifa nyingine naweza kusema zinafanana sana na simu ya mwaka jana ya Galaxy J7 (2017).

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sifa za Galaxy J7 (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.5 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 720 x 1280 pixels, 16:9 ratio (~267 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core,  chipset (Bado haijajulikana)
  • Uwezo wa GPU – Bado haijajulikana
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 au GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 256
  • Ukubwa wa RAM – GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 13
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nyeusi
  • Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM inayo Radio FM sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack
  • Ulinzi – Haina Fingerprint
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G

Kwa upande wa Galaxy J3 yenyewe inakuja na uwezo wa kawaida wa processor ya quad-core CPU yenye speed hadi GHz 1.4 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 2, Simu hii inakuja na kioo cha inch 5 chenye teknolojia ya IPS LCD Display. Battery ya simu hii inakuja ikiwa na uwezo wa 2,600 mAh. Sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.

Sifa za Galaxy J3 (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 720 x 1280 pixels, 16:9 ratio (~294 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53, Exynos 7570 Quad chipset
  • Uwezo wa GPU – Mali-T720
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 256
  • Ukubwa wa RAM – GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 2600 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
    pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue, Gold
  • Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM inayo Radio FM sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack
  • Ulinzi – Haina Fingerprint
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G

Bei ya Samsung Galaxy J7 (2018) na Galaxy J3 (2018)

Simu ya galaxy j7 (2018) bei yake bado haijajulikana, wakati Galaxy J3 (2018) yenye inakuja na ikiwa inauzwa kwa dollar za marekani $210 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 476,000. Kumbuka bei inaweza kuongezeka kutokana na kodi na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy J3 (2018) na J7 (2018)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment