Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Instagram Yaongezewa Video Chat, Kamera Effect na Mengine

Toleo hili linakuja pia na mtindo mpya wa kutafuta kwa urahisi
Instagram Feed Instagram Feed

Mtandao wa instagram umeanza kusasisha toleo jipya la App yake ya Instagram ambayo sasa inakuja na maboresho kadhaa kama vile uwezo wa kupiga simu za video hadi watu wanne, vikorobwezo vya kamera (Camera effect) pamoja na Sehemu mpya ya kutafuta (Explore feed).

  • Sehemu ya Video Chat 

Sehemu ya video chat inakuja kupitia sehemu ya Direct ambapo utaweza kupiga simu za video moja kwa moja kupitia app ya Instagram. Kupitia sehemu hii utaweza kupiga simu za video kwa mtu mmoja au kwa hadi kwa watu wanne kwa pamoja, kizuri zaidi ni kuwa baada ya kupiga simu unaweza kuendelea kuwasiliana kupitia simu za video huku unaperuzi mtandao wa Instagram. Ili kupiga simu ya video, unatakiwa kubofya kitufe cha kamera kilichopo juu upande wa kulia, kitufe hicho kinapatikana ndani ya chat zako na marafiki zako kupitia sehemu ya Direct (DM).

Advertisement

  • Kamera Effect

Kwenye toleo hili Instagram imeongeza baadhi ya vikorobwezo kwenye sehemu ya Stories sasa utaweza kupata Stika mpya, Effect mpya pamoja na aina mpya za vikorobwezo kutoka kwa watu mbalimbali maarufu.

  • Mtindo Mpya wa Sehemu ya Kutafuta (Explore Feed)

Toleo hili pia linakuja na mtindo mpya wa sehemu ya kutafuta, sehemu ambayo sasa inakuja na sehemu mpya ambayo imegawanyika kwa vipengele maalum kulingana na aina ya vitu unavyotaka kutafuta kupitia sehemu hiyo ya Instagram. Pia sehemu hiyo inakuja na sehemu mpya ya “For You” ambayo itakuonyesha picha na video mbalimbali ambazo zinalingana na akaunti yako.

Kwa sasa tayari sehemu hizi zote zinapatikana kupia App ya instagram za Android na iOS, kama bado hujaweza kuona sehemu hizi basi hakikisha una sasisha (update) app ya Instagram kupitia soko husika kati ya Play Store au App Store.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use