Facebook kupitia mtandao wake wa Instagram inasemekana kuwa inategemewa kuongeza idadi ya muda wa kupost video kwenye mtandao wake kutoka muda wa dakika moja hadi kufikia lisaa limoja. Kwa mujibu wa tovuti ya The Wall Street Journal, instagram inasemekana inategemea kufanya mabadiliko hayo ambayo yatasogeza mtandao huo wa instagram kukaribiana kufanana na mtandao wa YouTube pamoja na Facebook.
Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti hiyo, video hizo ndefu zinasemekana kuzingatia mfumo wa video za wima au (vertical video) kama ilivyo kwenye sehemu ya Stories. Hata hivyo bado hakuna ripoti kamili zilizo toleo na tovuti ya The Wall Street Journal, kama video hizo ndefu zitaruhusiwa kwenye sehemu ya Stories au kama zitaruhusiwa kwenye upande wa post za kawaida.
Kwa sasa watumiaji wa instagram wanaweza kuchapisha video za sekunde 15 kwenye sehemu ya Stories na sekunde 60 kwenye sehemu ya kawaida ya Feed. Hadi kufikia mwaka jana 2017 mwezi wa 11, Instagram ilikuwa na watumiaji wa sehemu ya Stories zaidi ya milioni 300 kwa siku, huku mtandao wa Instagram wenyewe ukiwa na jumla ya watumiaji zaidi ya milioni 800.
Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, wiki hii instagram imekuwa ikifanya maongezi na wabunifu mbalimbali pamoja na kampuni mbalimbali kuhusu uwezekano wa kuongeza urefu wa video kwenye mtandao huo wa Instagram.
Kwa sasa bado hakuna ripoti kamili kama instagram itawezesha watumiaji wa mtandao huo kuchapisha video hizo ndefu siku za karibuni hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi.