in

Tetesi : Instagram Kuzindua Sehemu Mpya Inayoitwa IGTV Leo

Sasa utaweza kupakia video ndefu zaidi kupitia mtandao wa Instagram

Instagram IGTV

Siku za karibuni tulipata ripoti kuhusu instagram kujiandaa na ujio wa sehemu mpya itakayo wawezesha watumiaji wake kupakia video ndefu kupitia mtandao wa Instagram. Kwa mujibu wa ripoti mpya kutoka kwenye tovuti ya Techcrunch, sehemu hiyo mpya inasemekana kuitwa IGTV.

Kwa mujibu wa mtandao huo sehemu hiyo itawaruhusu watumiaji wa mtandao wa Instagram kupakia video za muda mrefu na ambazo zitakuwa kwa mtindo wa wima. Mbali na hayo inasemekana pia watumiaji wataweza kuweka kava ambalo litakuwa likonyesha mwanzo wa video kama ilivyokuwa kwenye mtandao wa YouTube.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Hata hivyo ripoti zinasema kuwa sehemu hiyo pia itaweza kuwasaidia watumiaji wa mtandao huo kwa kuwalipa kiwango fulani cha pesa kutokana na matangazo yatakayo kuwa yakipita kwenye video kupitia sehemu hiyo ya IGTV. Bado hakuna ripoti kamili kiwango cha muda wa video hizo lakini inawezekana kuwa video zitakazowekwa kwenye sehemu hiyo zitakuwa na urefu wa dakika 10 au zaidi kwa mujibu wa ripoti kutoka mtandao wa Techcrunch.

Sehemu hii ya IGTV inasemekana kuzinduliwa siku ya leo kwenye mkutano utakao fanyika uko San Francisco nchini marekani kuanzia saa moja kamili ya usiku kwa saa za afrika mashariki. Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza yote yatakayojiri kwenye mkutano huo.

Tetesi : Instagram Kuzindua Sehemu Mpya Inayoitwa IGTV Leo
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.