in

Apps Nzuri za Kufuatilia kwa Karibu Kombe la Dunia

Unaweza kutumia app hizi kufuatilia michuano yote ya kombe la dunia

Apps Nzuri za Kufuatilia kwa Karibu Kombe la Dunia

Kuanzia mwezi huu, dunia inaungana pamoja kwenye ufunguzi wa michuano ya mpira wa miguu katika kuwania Kombe la Dunia, michuano hii hufanyika kila baada ya miaka 4, na kwa mwaka huu michuano hii inafanyika rasmi huko nchini Qatar.

Sasa ili kuhakikisha hupitwi na yoyote kwenye michuano hiyo, Tanzania Tech tumekuandalia application hizi nzuri ambazo unaweza kuzitumia ili kuhakikisha unafuatilia kombe la dunia wakati wowote.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Apps hizi nyingi zinapatikana kwenye mfumo yote yaani android na iOS hivyo kama wewe ni mtumiaji wa simu yoyote yenye mifumo hiyo basi unaweza kusoma makala hii ili kupata App ambayo kwako itakuwa ni rahisi kufuatili mechi hizi za kombe la dunia, bila kupoteza muda twende tukangalie app hizo.

2022 FIFA World Cup Official App

The Official FIFA App

App za kwanza kabisa kwenye list hii ni application za FIFA ambazo ni maalum kwa kombe la dunia, app hizi zitakupa habari zote, iwe ni picha video habari za ndani na nje ya uwanja pamoja na habari zingine zote zinazo husiana na kombe la dunia kwa ujumla. App hizi zinapatika kwenye mifumo yote ya Android na iOS.

FotMob World Cup

Application nyingine ya kusaidia kupata habari za kombe la dunia ni pamoja na App hizi za FotMob, app hizi pia ni nzuri sana na ni moja ya app ambazo watu wengi wamefurahia kuwa nazo mpaka sasa. Unaweza kupakua app hizi kwenye masoko yote ya Play Store na App Store.

World Cup App 2022 – Live Scores & Fixtures

App hii ni nzuri pia kwa kufuatilia kombe la dunia, lakini inapatikana kwenye mfumo wa android pekee kwa sasa, unaweza kupakua app hii kupitia soko la Play Store.

StarTimes – Live TV & Football

‎StarTimes ON
Price: Free+

App hizi ni app nyingine nzuri za kuwezesha wewe kujua yanayojiri kwenye michuano ya kombe la dunia huku nchini Qatar, App hii ni nzuri zaidi hasa kama uko kwenye nchi za Afrika. Pakua app hizi kupitia masoko yote ya Play Store pamoja na App store.

DStv Now

DStv
Price: Free
‎DStv Stream
Price: Free

Kwa wale wenye vingamuzi vya DSTV, app hizi ni muhimu sana hasa kama uko Afrika Mashariki, kwani kupitia App hizo utaweza kupata matangazo ya moja kwa moja ya michuano hiyo ya kombe kombe la duniani moja kwa moja kutoka Qatar kwa lugha ya Kiswahili. Unaweza kupakua app hizi kwenye masoko yote ya Play Store na App Store.

Na hizo ndio app nzuri ambazo zinaweza kukusaidia kuwa karibu na michuano hii ya kombe la dunia kupitia simu yako ya mkononi. Kama utashindwa kuwa na App yoyote kati ya hizi kwenye simu yako, unaweza kutumia Google kukupa taarifa zote kuhusu kombe hilo.

Unacho takiwa kufanya ni kutafuta kwa kuandika maneno haya “FIFA World Cup 2022” kwenye uwanja wa Google na utapata taarifa zote kuhusu michuano ya kombe la Dunia moja kwa moja kupitia Screen ya kifaa chako.

Na hizo ndio app nzuri kwaajili ya kombe la dunia kwa siku ya leo, Kama ulipitwa na list nyingine ya App nzuri unaweza kusoma list hiyo hapa. Kama una maoni kuhusu app nyingine nzuri ya kufuatilia kombe la dunia tafadhali tuandikie jina la app hiyo kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Apps Nzuri za Kufuatilia kwa Karibu Kombe la Dunia
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2024)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments