Video: Utani wa Samsung Galaxy S9 Kwa iPhone 6 na iPhone X

Ubunifu wa matangazo sambamba na utani kwa iPhone
utani wa Samsung kwa Apple utani wa Samsung kwa Apple

Siku hizi, ubunifu wa matangazo umekuwa mkubwa sana kuanzia gharama za kutengeneza tangazo hadi aina ya tangazo unalo tengeneza. Kifupi ni kuwa ubunifu wa matangazo umeenda next level hasa kwa wenzetu. Kama wewe ni mfuatiliaji wa maswala ya mtandao lazima utakuwa umeona tangazo jipya la Samsung Galaxy S9, kama bado hujaona tangazo hilo basi soma hii kisha angalia tangazo hilo hapo chini.

Tangazo hilo linautani kwa iPhone, likianza kwa kuonyesha mwanamke akiwa uwanja wa ndege na pale anapotaka kuonyesha tiketi yake ya ndege simu yake ya iPhone 6 inakuwa inachukua mda mrefu huku mtumiaji mwingine wa Galaxy S9 akionekana kuonyesha passport yake haraka bila tatizo na kupita.

Advertisement

Utani mwingine unaonyesha mwanamke huyo amesha ingia kwenye ndege na anataka kuangalia au kusikiliza kitu kwa kutumia simu yake ye iPhone 6, lakini bado simu yake hiyo inaonekana kuchukuwa muda kufungua programu. Pembeni yake kuna mtu anaonekana na simu ya Galaxy S9 Plus na yeye ana angalia video kwenye simu yake bila tatizo.

Mwanamke huyo anaonekana tena kashuka kwenye ndege na anataka kuchukua usafiri wa kulipia huku mvua inanyesha, na pale anapotaka kuchukua kuita usafiri kwa kutumia simu yake ya iPhone 6, bado simu yake inaonekana kuwa slow, anajikuta kaingia kwenye usafiri wa watu huku mwenye usafiri huo akiwa nje na simu ya Galaxy S9. Mwanamke huyo baadae anapata usafiri na akiwa njiani anaona duka la Apple na anaingia ndani na kumuomba msaidizi wa Apple amsaidie kurekebisha simu yake ili iwe inafanya kazi haraka.

Msaidizi huyo ana mwambie azime sehemu ya performance management feature, lakini pia ana mwambia akifanya hivyo simu yake ya iPhone 6 inaweza kuzima ghafla… Msaidizi huyo pia ana onekana aki mwambia mwanamke huyo au unaweza kununua simu mpya ya iPhone.

Baadae wanaonekana baba na mwana wakipishana na mwanamke huyo huku wamenyoa kama ukingo wa juu wa iPhone X, huku mwanamke huyo akiwashangaa. Baadae inaonekana mwanamke huyo ameamua kununua simu ya Galaxy S9 na kumtumia mtu meseji kwa kumwambia amefanikiwa kubadilisha simu.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use