in

Programu ya Siri Kuongezewa Sauti Mpya Mwezi Ujao

Jiandae na mambo mapya kupitia mkutano wa Apple WWDC

Siri Apple

Kampuni ya Apple ipo mbioni kufanya mkutano wake wa kila mwaka unaojulikana kama WWDC auĀ Apple Worldwide Developers Conference, mkutano huu uhusisha wabunifu mbalimbali wa programu na bidhaa za Apple na mara nyingi kwenye mkutano huu Apple huonyesha bidhaa mpya pamoja na maboresho ya bidhaa zake za awali.

Moja ya maboresho yanayo tarajiwa siku za karibuni ni pamoja na Programu ya siri kuongezewa sauti mpya. Kwa mujibu wa tovuti ya The next web, Programu ya siri yenyewe ndio imetoa siri hiyo, na unaweza kujaribu kama unatumia simu ya iPhone au iPad yenye uwezo wa programu ya Siri, unaweza kuuliza programu hiyo kwa kusema “Tell Me About WWDC”.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Mbali na hayo inawezekana kuwa Apple itazindua spika janja mpya kwenye mkutano wa WWDC, simu mpya ya iPhone SE 2, pamoja na mambo mengine mengi kuhusu mfumo mpya wa uendeshaji wa iOS na MacOS. Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha yote yatakayojiri kwenye mkutano huo unaotarajiwa kuanzia rasmi tareheĀ 4, mwezi wa sita 2018, hadi tarehe 8 June 2018.

Programu ya Siri Kuongezewa Sauti Mpya Mwezi Ujao
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Simu Yako (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.