Mwaka jana Instagram ilitangaza ujio wa stika maalum za uchaguzi maarufu kama (Poll Stickers), Stika hizo zimekuwa sehemu muhimu kwa watu mbalimbali kupata majibu ya maswali kupitia mtandao wa Instagram. Tokea stika hizi zilipoletwa kwenye app ya Instagram mpaka sasa, watumiaji wa Instagram walikuwa wakitumia aina moja tu ya stika iliyokuwa na sehemu ya kubofya ndio au hapa.
Kwa mujibu wa blog ya instagram, Sasa Instagram imeleta aina mpya ya Stika ya emoji ambayo itakusaidia kupata majibu ya maswali yako mbalimbali ndani ya mtandao wa Instagram. Aina hiyo mpya itakupa uwezo wa kupata majibu ya maswali yako kwa kutumia emoji unayoweza kuweka sambamba na swali lako.
Kwa mfano kama unataka kuuliza swali kama “unaonaje tovuti ya Tanzania Tech ?” hapa utaweza kuchagua picha unayotaka kuuliza swali, kisha utachagua sehemu ya Stika, baada ya hapo utaona aina hiyo mpya ya Stika yenye emoji kisha andika swali lako alafu chagua aina ya emoji unayotaka kisha tuma au post picha hiyo. Sasa baada ya kupost kwa upande wa mpiga kura atakuwa na uwezo wa kutoa majibu kwa kusogeza emoji hiyo mpaka pale anapo ona ni sahihi na hapo ataweza kupiga kura moja kwa moja.
Kwa upande wa majibu, mwenye swali ataweza kuona mstari wenye sura ya emoji aliyo ichagua awali ambao itakuwa ikiashiria jumla ya majibu kulingana na watu walio piga kura kwenye swali hilo pamoja na mistari mingine kwenye majina ya watu walio piga kura kwenye swali lake ikiwa ina onyesha idadi ya kura kwa kila mtu alizotoa kwenye swali hilo.
Kwa sasa sehemu hii tayari inapatikana kwenye App za Instagram za Android na iOS kama bado hujapata sehemu hii hakikisha una update Application yako ya instagram kisha jaribu sehemu hiyo kwa kufuata hatua hapo juu.