Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 5.1, Nokia 3.1 na Nokia 2.1

Zifahamu sifa za Simu Mpya za Nokia 5.1, Nokia 3.1 na Nokia 2.1
Simu Mpya za Nokia 5.1 Nokia 3.1 na Nokia 2.1 Simu Mpya za Nokia 5.1 Nokia 3.1 na Nokia 2.1

Siku ya jana kampuni ya Nokia kupitia HMD Global, ilitangaza ujio wa matoleo mapya ya simu zake za Nokia 5, Nokia 3 pamoja na Nokia 2. Matoleo hayo ya Nokia 5.1, Nokia 3.1 na Nokia 2.1 yanakuja na maboresho macheche tofauti matoleo ya kwanza ya simu zilizo tangulia.

Nokia 5.1

Advertisement

Nokia 5.1 imeongezewa kioo kikubwa cha inch 5.5 chenye teknolojia ya Full HD IPS LCD chenye resolution ya 1080 x 2160 pixel pamoja na aspect ratio ya 18:9 na ulinzi wa Gorilla Glass 2.5D. mbali na hayo Nokia 5.1 ni nyembamba kidogo zaidi ya Nokia 5. Maboresho mengine ya Nokia 5.1 ni pamoja na kamera ya Megapixel 16 kwa nyuma huku kwa mbele ikiwa na kamera ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 8.

Simu hii inakuja na ukubwa wa ndani wa aina mbili wa GB 16 na GB 32 huku ukiwa na uwezo wa kuongezeka kwa kutumia Memory Card. Kwa upande wa RAM Nokia 5.1 inakuja ikiwa na machaguo mawili pia ya RAM kati ya simu yenye RAM ya GB 2 na RAM ya GB 3.

Nokia 3.1

Kwa upande wa Nokia 3.1, yenyewe nayo inakuja na maboresho ya kioo kwa kuongezewa kioo chenye ukubwa wa inch 5.2 IPS chenye resolution ya 720p+, mbali na hayo simu hiyo pia imeongezewa uwezo wa processor kwa kuwa na processor ya MediaTek 6750 chipset yenye uwezo wa Cortex-A53 cores. Kwa upande wa ukubwa wa ndani pamoja na RAM, Nokia 3.1 inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 16 pamoja na RAM ya GB 2, toleo lingine lita kuwa na RAM ya GB 3 na ukubwa wa ndani wa GB 32.

Nokia 2.1

Kwa upande wa Nokia 2.1 yenyewe inakuja ikiwa inatumia mfumo wa uendeshaji wa Android Go na inakuja na kioo kilicho ongezwa cha inch 5.5 ambacho kinakuja na resolution ya 720p pamoja na aspect ratio ya 16:9. Kama kawaida ya simu zinazotumia mfumo wa Android Go, Nokia 2.1 inakuja na RAM ya GB 1 na ukubwa wa ndani wa GB 8, Battery ya simu ina uwezo wa 4,000 mAh ambayo inauwezo wa kudumu siku mbili. Kamera za simu hii zinakuja zikiwa na Megapixel 8 kwa nyuma na Megapixel 5 kwa mbele, simu hii inakuja kwa machagua ya rangi za Blue/Copper, Blue/Silver pamoja na Gray/Silver.

Bei za Nokia 5.1, Nokia 3.1 na Nokia 2.1

Kwa upande wa bei za simu hizi, Nokia 5.1 inakuja ikiwa inauzwa dollar $219 sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 500,000. Nokia 3.1 yenyewe itakuja ikiwa inauzwa dollar za marekani $159 sawa na Tsh 363,000. Nokia 2.1 itakuja ikiwa inauzwa kwa dollar za marekani $115 sawa na Tsh 263,000. Kumbuka kwa Tanzania bei za simu hizi zinaweza kubadilika kutokana na kodi pamoja na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use