Soma Hapa Kujua Bei na Sifa za Simu Mpya ya One Plus 6

Kama wewe ni mpenzi wa simu za One Plus basi ni muhimu sana kusoma hii
Sifa na bei ya One Plus 6 Sifa na bei ya One Plus 6

Hapo Jana kampuni ya kutengeneza simu ya One Plus ya nchini china ilizindua simu yake mpya ya One Plus 6, simu hiyo inasemekana kuwa ndio simu bora zaidi kutoka kampuni hiyo ukizingatia hiyo ndio simu ya saba kuzinduliwa na kampuni ya One Plus tokea kampuni hiyo ilipoanzishwa rasmi na Pete Lau na Carl Pei mwaka 2013.

Pamoja na hayo simu hii pia ndio simu ya bei ghali zaidi kutoka kampuni hiyo ukilinganisha na simu nyingine ambazo zimewahi kutolewa na kampuni hiyo. Hata hivyo, sababu za simu hii kuwa ya bei ghali zaidi kutoka kampuni hiyo anazo mmoja wa wagunduzi wa kampuni ya One Plus ambaye alihojiwa na waandishi wa tovuti ya CNET na kwenye mahojiano hayo alisikika akisema “muundo huu wa simu ya One Plus 6 ndio muundo bora zaidi wa simu kutoka kampuni ya One Plus hivyo ni lazima utakuwa na gharama kidogo” Alisema Carl Pei.

Advertisement

Sifa za One Plus 6

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.28 chenye teknolojia ya Optic AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, 19:9 ratio (~402 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 4×2.8 GHz Kryo 385, Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipest.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja itakuwa na GB 128 nyingine GB 256 na nyingine itakuwa na uwezo wa GB 64 zote zikiwa hazina sehemu ya kuweka Memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Machaguo mawili RAM ya GB 6 na nyingine itakuwa na RAM ya GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye (f/2.0, 20mm, 1/3″, 1.0µm), gyro-EIS, Auto HDR, 1080p.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko Mbili moja ina Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/1.7, 27mm, 1/2.6″, 1.22µm, gyro-EIS, OIS) na nyingine yenye Megapixel 20 yenye (f/1.7, 1/2.8″, 1.0µm), kamera zote zina uwezo wa phase detection autofocus, dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3300 mAh battery yenye uwezo wa – Fast battery charging 5V 4A 20W (Dash Charge).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 5.0, A2DP, LE, aptX HD pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Midnight Black, Mirror Black na Silk White.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa Nyuma)

Bei ya One Plus 6

Kwa upande wa bei One Plus 6 itauzwa kwa bei ya dollar za marekani $529 kwa One Plus 6 yenye GB 64 ambayo ni sawa na Tsh 1,210,000 na One Plus 6 ya GB 128 yenyewe itauzwa kwa dollar $579 sawa na Tsh 1,322,000, Huku One Plus 6 ya GB 256 yenyewe itauzwa kwa dollar $629 sawa na Tsh 1,436,000. Kumbuka bei hizo ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo, hivyo bei inaweza kubadilika kwa Tanzania ukichanganya na kodi.

Tuambie kwenye maoni hapo chini unaonaje muundo na sifa za simu hii mpya ya One Plus 6..? Je bei yake inaendana na muundo na sifa za simu hii..? Tuambie kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

1 comments
  1. Nimeona swali la mdau mmoja kuhusiana na simu zinazonunuliwa Dubai… utakuta eneo la hardware version limeandikwa
    United Arab Emirates
    TRA ID:0016333/08
    TA:00000000/00
    1.nini maana yake na
    2. huwa software update haipokei.
    Je nini cha kufanya ili ziweze kupokea software update
    T

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use