Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei za Simu Mpya za LG Q7

Sifa na Bei za Simu mpya za LG Q7, LG Q7 Plus na LG Q7 Alpha
Sifa za LG Q7 Sifa za LG Q7

Kama wewe ni msomaji wa Tanzania Tech lazima utakuwa umegundua kuwa wiki hii habari za simu mpya zimekua nyingi sana, tumeona jana Samsung ikizindua simu zake mpya za Galaxy J Series pamoja na Samsung Galaxy S Light Luxury au kama wengi nanavyo sema Galaxy S8 Lite.

Sasa shughuli ya ujio wa simu mpya bado haijaisha kwani siku ya jana pia kampuni ya LG ilizindua simu yake mpya ya LG Q7, Tofauti na simu nyingine za LG simu hii imekuja na maboresho zaidi kwa upande wa sauti. Simu hii inakuja na teknolojia ya Hi-Fi audio yenye DTS:X 3D Surround Sound ambayo inauwezo wa kutoa sauti ya 7.1 channels kwenye headphone. Yaani kifupi ni kwamba simu hii inakuja na sauti ya kipekee sana.

Mbali na hayo LG Q7 imetengenezwa kwa kava la kisasa la chuma ambalo lina ipa simu hiyo uwezo wa kuzuia simu hiyo isiingie maji, Simu hii pia inakuja na kioo cha inch 5.5 chenye teknolojia ya Full Vision LCDs chenye resolution ya 1080p (18:9, 2,160 x 1,080 px). Simu hizi zinatoka zikiwa za aina tatu yaani LG Q7, LG Q7 Plus na LG Q7 Alpha. Sifa za simu hizo ni kama zifuatazo.

Advertisement

Sifa za LG Q7, LG Q7 Plus na LG Q7 Alpha

  • Ukubwa wa Kioo  – Simu zote zina kioo cha Inch 5.5 chenye teknolojia ya IPS LCD display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~439 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Simu zote zina Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.5 GHz Cortex-A53 au Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53, Chipset (Bado Haijajulikana)
  • Uwezo wa GPU – (Bado Haijajulikana)
  • Ukubwa wa NdaniLG Q7 itakuja na ukubwa wa ndani wa GB 32, LG Q7 Plus itakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 na LG Q7 Alpha itakuja na ukubwa wa ndani wa GB 32 zote zitaweza kuongezewa ukubwa kwa kutumia Memory card hadi ya GB 400.
  • Ukubwa wa RAMLG Q7 itakuja na RAM ya GB 3, LG Q7 Plus itakuja na RAM ya GB 4 na LG Q7 Alpha itakuja na RAM ya GB 3.
  • Uwezo wa Kamera ya MbeleLG Q7 itakuja na Kamera ya mbele ya Megapixel 8, LG Q7 Plus itakuja na kamera ya Megapixel 8 na LG Q7 Alpha itakuja na Kamera ya Megapixel 5.
  • Uwezo wa Kamera ya NyumaLG Q7 itakuja na Kamera ya nyuma ya Megapixel 13, LG Q7 Plus itakuja na kamera ya Megapixel 16 na LG Q7 Alpha itakuja na Kamera ya Megapixel 13, Kamera za nyuma za simu zote zinayo phase detection autofocus pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Simu zote zina Battery isiyotoka ya Li-Po 3000 mAh battery.
  • Viunganishi – Simu zote zina Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, 2.0, Type-C 1.0 reversible connector
  • Rangi – Simu zote zinakuja kwa rangi tatu za Aurora Black, Moroccan Blue na Lavender Violet.
  • Mengineyo – Simu zote zina Radio FM, Zinatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), zinayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Simu zote zinayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Simu za LG Q7, LG Q7 Plus na LG Q7 Alpha

Kwa mujibu wa tovuti ya LG, Kwa upande wa bei ya simu hizi bado haijatangazwa rasmi hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha rasmi pindi bei ya simu hizi itakapo Tangazwa rasmi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use