Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, sasa the wait is over..! Kampuni ya LG hapo siku ya jana imetambulisha rasmi simu yake mpya ya LG G7 ThinQ. Kama zilivyo simu nyingi za mwaka 2018 simu hii mpya ya LG G7 ThinQ inakuja na kioo cha inch 6.1 pamoja na ukingo wa juu maarufu kama (top notch) bila kusahau mfumo wa AI kwenye kamera.
Kama umeangalia video hapo juu sidhani kama kuna haja ya kukueleza maboresho yaliyomo kwenye simu hii, basi kwa sababu hiyo ngoja tuangalie sifa za simu hii moja kwa moja.
Sifa za LG G7 ThinQ
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.1 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 3120 pixels, 19.5:9 ratio (~564 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo), planned upgrade to Android 9.0 (P)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver), Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipest.
- Uwezo wa GPU – Adreno 630
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 128 na nyingine itakuwa na uwezo wa GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 6 na nyingine itakuwa na GB 4
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye (f/1.9).
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko Mbili moja ikiwa na Megapixel 16 (f/1.6, OIS, laser & PDAF) na nyingine ikiwa na Megapixel 16 (f/1.9) zote zikiwa na laser & phase detection autofocus pamoja na LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3000 mAh battery, yenye uwezo wa Fast battery charging (Quick Charge 3.0)
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go
- Rangi – Inakuja kwa rangi nne za New Platinum Gray, New Aurora Black, New Moroccan Blue pamoja na Raspberry Rose.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Haingizi Maji wala Vumbi.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa Nyuma)
Kwa upande wa bei bado kampuni ya LG haijatangaza bei halisi ya simu hii, endelea kutembelea ukurasa huu tutaongeza bei pindi kampuni ya LG itakapo tangaza bei ya simu hii.
Bei ikiwa tayari tujuze Ttech
Na tuinunie wapi
Karibu kaka, tutafanya hivyo.