Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Nini Maana ya GDPR (General Data Protection Regulation)

Kama umekuwa na maswali mengi hii ndio maana ya GDPR
Nini Maana ya GDPR Nini Maana ya GDPR

Kama wewe ni mtumiaji wa tovuti mbalimbali, basi lazima umekutana na neno (GDPR), Japo kuwa neno hili limekuwa linatumika sana kipindi hichi, lakini ni watu wachache sana hasa hapa Tanzania wanajua maana halisi ya neno hili.

Maana ya GDPR ni (General Data Protection Regulation), hii ni sheria mpya ya mtandao ambayo inatumika kwa wamiliki wote wa tovuti nchini ulaya au wenye tovuti zinazofanya kazi nchini ulaya. Sheria hii inawataka wamiliki wa tovuti nchini Ulaya au wenye tovuti zinazofanya kazi nchini ulaya kuonyesha jinsi wanavyo tumia data wanazo zikusanya kutoka kwa watumiaji wa tovuti hizo. Tunaposema “data zinazo kusanywa” hapa tuna maana, hizi ni zile data zinazopatikana baada ya mtumiaji wa tovuti kujisajili na tovuti, kutoa maoni kwenye makala, au kujisajili ili kupata habari kwenye barua pepe.

Advertisement

Kwa kupitia sheria hiyo ya mtandao ya ulaya, mmiliki wa tovuti inayofanya kazi nchini ulaya analazimika kuhakikisha ana onyesha ni jinsi gani anatumia data alizo zikusanya kutoka kwa watumiaji wake na ni kwanini mtumiaji analazimika kutoa data hizo ili kutumia tovuti husika. Mbali na hayo pia sheria hizo zinamtaka mwenye tovuti inayofanya kazi ulaya au iliyoko ulaya, kutoa uhuru wa mtumiaji kufuta data zake kwenye tovuti husika au kufanya marekebisho ya data zake pale anapo hisi zimekosewa

Hivyo basi kama wewe unayo tovuti yoyote ambayo unahisi kwa namna moja ama nyingine inaweza kutumiwa na watu wa nchi za ulaya, basi ni lazima kuhakikisha unazi fuata sheria hizo na kutii sheria hizo kuanzia tarehe 25 ya mwezi May mwaka 2018. Kwa kukiuka sheria hizo utaweza kupigwa faini au kufungo cha jela au tovuti yako kufungiwa au vitu vyote kwa pamoja.

Kama tovuti yako au huduma unayotoa mtandaoni, haiusishi nchi za ulaya basi unaweza kuendelea kutoa huduma yako mtandaoni bila kuwa na ulazima wa kufuata sheria hizo, lakini kama unahisi kwa namna yoyote tovuti au huduma unayo itoa mtandaoni inahusisha kwa namna yoyote wananchi wa nchi za ulaya basi hakikisha tovuti yako ina fuata sheria hizo.

Muhimu wa sheria hii unakuja zaidi kama tovuti yako inayo mfumo wa kujisajili ambao mara nyingi mfumo huu hutumia barua pepe au namba ya simu. Vilevile kama tovuti yako inatumia huduma zinazo saidia kujua jinsi watumiaji wanavyo tumia tovuti yako kama vile (Google Analytics) pamoja na huduma za matangazo kama (Google Adsense) na nyingine kama hizo ambazo zinakusanya data za watumiaji kwa namna moja ama nyingine, basi ni lazima pia kuhakikisha tovuti yako inafuta sheria hizo.

Kujua zaidi kuhusu sheria hizo na jinsi zinavyo walinda wananchi wa nchi za ulaya unaweza kusoma hapa ili kujua zaidi. Hivyo wakati mwingine unakutana na barua pepe akionyesha maswala ya Privacy Policy au GDPR, basi moja kwa moja elewa kwamba hiyo ni kwa sababu ya sheria hiyo mpya ambayo imeanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jana tarehe 25 mwezi May 2018.

Mpaka hapo natumaini umepata mwanga kidogo kuhusu GDPR au (General Data Protection Regulation), kama una maswali au maoni basi unaweza kuuliza kupitia kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use