Aliye Gundua WhatsApp Atangaza Kuachana na Facebook

Bado hakuna sababu kwanini mgunduzi huyo amefikia uamuzi huo
Jan Koum Jan Koum

Habari mpya mtandaoni leo zinasema, mmoja wa waguduzi wa programu ya WhatsApp Jan Koum ametangaza rasmi kuachana na kampuni ya Facebook.

Mwanzoni baada ya Facebook kununua programu ya WhatsApp kutoka kwa wagunduzi wake Jan Koum na Brian Acton, wawili hao waliendelea kufanyia kazi programu hiyo wakiwa chini ya kampuni ya Facebook, lakini ilipofikia mwanzoni mwa mwaka huu mmoja wa wagunduzi hao, Brian Acton alitangaza kuachana rasmi na kampuni ya Facebook na kumuacha mgunduzi mwenzake akiendelea kufanya kazi chini ya kampuni ya Facebook, miezi michache baadae mgunduzi huyo naye ametangaza rasmi kuachana na kampuni ya hiyo.

Advertisement

Akielezea kwenye post aliyoituma kupitia mtandao wa Facebook, Jan Koum amesema kuwa ni mda mrefu umepita kutoka yeye na Brian Acton walipo gundua programu hiyo na kutoka kipindi hicho mpaka sasa amefanikiwa kufanya kazi na baadhi ya watu ambao anashukuru kufanya nao kazi lakini sasa muda wake umefika kuachana na programu hiyo na kufanya mambo mengine ambayo ni pembeni ya teknolojia.

Hata hivyo, mgunduzi huyo akueleza sababu za kuachana na kampuni ya Facebook lakini wachambuzi wa maswala ya teknolojia wanasema, Jan Koum ameachana na kampuni hiyo kwa sababu ya kuwa na kuto ku-kubaliana na baadhi ya mambo yanayo fanywa na kampuni ya Facebook ambayo yana semekana ni kinyume na watumiaji wa programu hiyo.

Kwa upande wake Mark Zuckerberg aliandika kwa kujibu post ya mugunduzi huyo kuwa, ana sikitika kumpoteza mtu makini kama Jan Koum na ataendelea kukumbuka ufanyaji wake wa kazi wa karibu na pia ataendelea kumshukuru kwa kumfundisha mambo mbalimbali ikiwa pamoja na maswala ya ulinzi na mambo mengine, pia mark aliandika ataendelea kufanyia kazi mambo hayo na yata endelea kuwa moyo wa programu ya WhatsApp.

Haya yanakuja wakati ni wiki chache kutoka Mark Zuckerberg alipo simama mbele ya Congress au wabunge wa marekani na kujibu maswali magumu kuhusu usalama wa watumiaji wa mtandao huo nchini humo baada ya sakata la uvujishaji data la Cambridge Analytica.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use